Back to Languages

Swahili - Chapter 106 - Quraysh

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Quraysh 106:1

Oneni ajabu ya mazowea ya Makureshi, amani walionayo, kuwaendea uzuri mambo yao

Verse 2 — Surah Quraysh 106:2

kupangika na kusahilika misafara yao ya kwenda Yamani kipindi cha kusi na kwenda Shamu kipindi cha kaskazi, ili kuleta vitu wanavyohitajia

Verse 3 — Surah Quraysh 106:3

Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada

Verse 4 — Surah Quraysh 106:4

Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na kicho kikubwa na babaiko