Back to Languages

Swahili - Chapter 113 - Al-Falaq

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Falaq 113:1

Sema, ewe Mtume, «Najilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa asubuhi

Verse 2 — Surah Al-Falaq 113:2

«Kutokana na shari la viumbe na udhia wao

Verse 3 — Surah Al-Falaq 113:3

«Na shari la usiku wenye giza lingi ungiapo na ujikitapo na mashari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake

Verse 4 — Surah Al-Falaq 113:4

«Na shari la wchawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga

Verse 5 — Surah Al-Falaq 113:5

«Na shari la hasidi mwenye kutukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Aliyewaneemesha ziwaondokee.»