Anaepushwa na Qur’ani na Mtume yule aliyeepushwa na lile la kuviamini hivyo viwili kwa kuzipa mgongo dalili za Mwenyezi Mungu na hoja Zake za yakini, na kwa hivyo haafikiwi kwenye kheri
Hakika ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo makubwa na chemchemi za maji yenye kutembea. Mwenyezi Mungu Atawapa yote wanayoyatamani ya aina mbalimbali za starehe
Watazipokea neema hizo wakiwa wameridhika nazo na nafsi zao zina furaha. Hakika wao, kabla ya kupata sterehe hizo, walikuwa wema duniani kwa matendo yao mema
Na katika ardhi kuna mazingatio na dalili waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, Aliye Peke Yake na asiye na mshirika, na wenye kumuamini Mtume Wake. rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
Na katika kuwaumba nyinyi kuna dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na kuna mazingatio ya kuwaonyesha nyinyi upweke wa Muumba wenu na kwamba Yeye hakuna Mola Anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Je, mumeghafilika na hilo mkawa hamlioni mkazingatia kwalo
na walikuwa ni miongoni mwa Malaika watukufu- wakati walipomjia nyumbani kwake, wakamwamkia kwa kumwambia, «Salama!»Akawarudishia maamkizi kwa kusema, «Salama ni kwenu! Nyinyi ni watu wageni hatuwajui.»
Alipowaona hawali aliingiwa na kicho cha kuwaogopa, na hapo wakamwambia, «Usiogope! Sisi ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu. Na wakampa bishara kwamba mkewe Sarah atamzalia mtoto atakayekuwa ni miongoni mwa watu wanaomjua Mwenyezi Mungu na kuijua Dini Yake, naye ni Isḥāq, amani imshukie
Aliposikia mke wa Ibrāhīm maneno ya bishara ya hao Malaika, alielekea upande wao na ukelele, akajipiga uso wake kwa kulionea ajabu jambo hili na akasema, «Vipi nitazaa na mimi ni tasa sizai?»
Malaika wa Mwenyezi Mungu wakamwambia, «Hivyo ndivyo Alivyosema Mola wako kama tulivyokwambia. Na Yeye Muweza wa hilo, hapana la ajabu kutokana na uweza Wake. Hakika Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mwenyew hekima Anayeviweka vitu mahali pake, Ndiye Mwenye kuyajua maslahi ya waja Wake
Na tukaacha kwenye mji huo uiliotajwa athari iliyosalia ya adhabu iwe ni alama ya uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na vile alivyowatesa makafiri. Ili hilo liwe ni zingatio kwa wale wanaoiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyo kali na yenye kuumiza
Na kuhusu mambo ya watu wa kabila la 'Ād na kuwaangamiza wao kuna dalili na mazingatio kwa mwenye kutia mambo akilini, tulipowapelekea wao upepo usiokuwa na baraka na usioleta kheri yoyote
Na kuhusu watu wa kabila la Thamūd na kuangamizwa kwao kuna dalili na mazingatio, walipoambiwa-na msemaji hapa ni Nabii wao Ṣāliḥ, amani imshukie-, «Jistarehesheni mjini kwenu siku tatu mpaka muda wenu wa kuishi ukome
Na tuliwaangamiza watu wa Nūḥ kabla ya hawa, hakika wao walikuwa ni watu wenye kuenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kutoka nje ya utiifu Kwake
Na mbingu tuliziumba na tukazitengeneza vizuri, na tukazifanya ni sakafu ya ardhi kwa nguvu na uweza mkubwa, na sisi tutayapanua maeneo yake na pande zake
Basi kimbieni, enyi watu , kutoka kwenye mateso ya Mwenyezi Mungu na muelekee kwenye rehema Yake kwa kumuamini Yeye na Mtume Wake, kufuata amri Yake na kufanya mambo ya utiifu Kwake. Hakika mimi, kwenu nyinyi, ni muonyaji ambaye maonyo yake yako waziwazi. Na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikuwa akizungukwa na mambo hukimbilia Swala, na huku ndiko kumkimbilia Mwenyezi Mungu
Kama walivyomkanusha Makureshi Mtume wao Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakasema, «Yeye ni mshairi, au mchawi, au mwendawazimu.», ndivyo walivyofanya ummah waliowakanusha Mitume wao kabla ya Makureshi, na Mwenyezi Mungu Akawashushia mateso Yake
Je, waliusiana wa mwanzo na wa mwisho kumkanusha Mtume waliposema hivyo kwa umoja wao? Bali wao ni watu wenye kukiuka mipaka kwa uhalifu, nyoyo zao zimefanana na vitendo vyao kwa ukafiri na ukiukaji mipaka, ndipo waliokuja nyuma wakasema hayo kama walivyosema waliotangulia
Wapuuze hao washirikina, ewe Mtume, mpaka itakapokujia wewe amri ya Mwenyezi Mungu kuhusu wao, hapatakuwa na yoyote mwenye kukulaumu, kwani ushafikisha yale uliyotumilizwa kwayo
Pamoja na kuwapuuza wao, ewe Mtume, na kutoshughulika na ufidhuli wao, endelea kuwaidhia wale uliotumilizwa kwao, kwani kukumbusha na kuwaidhia watanufaika nako wale wenye nyoyo zenye kuamini, na katika kufanya mawili hayo kuna kusimamisha hoja kwa wenye kupa mgongo
Sitaki kutoka kwao riziki wala sitaki wanilishe, kwani mimi Ndiye Mpaji Mwenye kuruzuku. Kwani Yeye, Aliyetakasika na kila sifa za upungufu, hawahitaji viumbe Vyake, bali wao ndio wahitaji Kwake katika hali zao zote, Yeye Ndiye Mwenye kuwaumba na kuwaruzuku na Aliyejikwasisha nao kwa kutowahitajia
Hakika Mwenyezi Mungu , Peke Yake, Ndiye Mwenye kuviruzuku viumbe Vyake, Ndiye Anayedhamini chakula chao, Mwenye nguvu Aliye Thabiti, Hatendeshwi nguvu wala hakuna Mwenye kushindana Naye. Ni Wake Yeye uweza wote na nguvu
Hakika wale waliodhulumu kwa kumkanusha kwao Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wana fungu la adhabu ya Mwenyezi Mungu mfano wa fungu la wenzi wao waliopita kabla yao. Basi wasiifanyie haraka adhabu , kwani hapana budi ni yenye kuwajia
maangamivu na usumbufu ni wa wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kutokana na Siku yao wanayoahidiwa kuteremkiwa na adhabu, nayo ni Siku ya Kiyama