Back to Languages

Swahili - Chapter 73 - Al-Muzzammil

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Muzzammil 73:1

Ewe ulijifinika nguo zako

Verse 2 — Surah Al-Muzzammil 73:2

Inuka uswali kipindi cha usiku isipokuwa sehemu chache yake

Verse 3 — Surah Al-Muzzammil 73:3

Inuka kwa muda wa nusu ya usiku au kupungua nusu kidogo mpaka ufikie theluthi

Verse 4 — Surah Al-Muzzammil 73:4

Au ongeza zaidi ya nusu mpaka ufikie theluthi mbili. Na usome Qur’ani kwa utaratibu na utulivu, uzifafanue herufi na vikomo

Verse 5 — Surah Al-Muzzammil 73:5

Hakika sisi tutakuteremshia, ewe Nabii, Qur’ani tukufu inayokusanya maamrisho na makatazo na hukumu za kisheria

Verse 6 — Surah Al-Muzzammil 73:6

Hakika ibada inayo inayofanya ndani ya usiku ina athari kubwa zaid moyoni, na maneno yanabainika zaidi, kwa kuwa moyo uko mtupu hauna mashughuli ya kilimwengu

Verse 7 — Surah Al-Muzzammil 73:7

Hakika wewe katika kipindi cha mchana una wakati wa kuzunguka na kushughulika katika mambo yenye maslahi nawe na kufanya harakati nyingi kwa majukumu ya utume, basi wakati wa usiku ipe nafasi nafsi yako kumuabudu Mola wako

Verse 8 — Surah Al-Muzzammil 73:8

Na ulitaje, ewe Nabii, jina la Mola wako, umuombe kwalo na utindikie Kwake kikamilifu katika ibada yako na ujitegemeze Kwake

Verse 9 — Surah Al-Muzzammil 73:9

Yeye Ndiye Mmiliki wa Mashariki na Magharibi. Hakuna muabudiwa ka haki isipokuwa Yeye. Basi mtegemee Yeye na umuachie Yeye mambo yako

Verse 10 — Surah Al-Muzzammil 73:10

Na uvumilie kwa yale ambayo washirikina wanayasema kuhusu wewe na kuhusu Dini yako. Na uende kinyume na wao katika maneno yao ya ubatilifu pamoja na kuwapuuza na kuacha kuwalipiza

Verse 11 — Surah Al-Muzzammil 73:11

Na uniache mimi, ewe Mtume, na hawa wakanushaji wa aya zangu, wenye starehe na gogi la ulimwengu, na uwape muhula wa muda mchache kwa kucheleweshewa adhabu mpaka muda wa wao kuadhibiwa ufikie ukomo wake

Verse 12 — Surah Al-Muzzammil 73:12

Kwa hakika wao watapata kwetu sisi huko Akhera pingu nzito na Moto wenye kuwaka ambao watachomwa nao

Verse 13 — Surah Al-Muzzammil 73:13

na chakula cha kuchukiza chenye kusakama kooni kisicho na ladha, na adhabu inayoumiza

Verse 14 — Surah Al-Muzzammil 73:14

Siku itakapotikisika na kusukikasukika ardhi na majabali mpaka majabali yawe mlima wa mchanga wenye kutiririka na kupeperuka, baada ya kuwa kwenye hali ya ugumu na ukavu

Verse 15 — Surah Al-Muzzammil 73:15

Hakika sisi tumemtumiliza kwenu nyinyi, watu wa Makkah, Muhammad kuwa ni Mtume, mwenye kutoa ushahidi wa ukafiri na uasi unaotokana na nyinyi, kama vile tulivyomtumiliza Mūsā kuwa ni Mtume kwenda kwa Fir’awn aliyepita kiasi katika uasi

Verse 16 — Surah Al-Muzzammil 73:16

Basi Fir’awn akamkanusha Mūsā na asiukubali utume wake, na akakataa amri yake, tukamuangamiza maangamivu makali. Hapa pana onyo la kumuasi Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kuogopea isije ikamfika yule aliyeasi mfano wa kile kilichomfika Fir‘awn na watu wake

Verse 17 — Surah Al-Muzzammil 73:17

Vipi mtajikinga nafsi zenu, mkikufuru, na adhabu ya Siku ya Kiyama ambayo huwafanya watoto wadogo watokwe na mvi kwa ukubwa wa janga lake na unguliko lake

Verse 18 — Surah Al-Muzzammil 73:18

Mbingu zitakuwa na pasuko Siku hiyo, kwa ukubwa wa janga lake, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ya kuwa Siku hiyo itakuja ni yenye kutukia bila shaka

Verse 19 — Surah Al-Muzzammil 73:19

Hakika aya hizi zenye kutisha ambazo ndani yake kuna vigongaji na vikemeaji ni mawaidha na mazingatio kwa watu. Basi mwenye kutaka kuwaidhika na kunufaika nazo, na achukue utiifu na uchamungu kuwa ni njia ya kumfikisha kwenye radhi za Mola wake Aliyemuumba na kumlea

Verse 20 — Surah Al-Muzzammil 73:20

Hakika Mola wako, ewe Mtume, Anajua kuwa wewe unasimama kwa swala ya Tahajudi kipindi cha usiku, wakati mwingine chini ya theluthi mbili za usiku, na wakati mwingine unasimama nusu yake, na wakati mwingine theluthi yake. Na wanasimama pamoja na wewe kundi la Maswahaba wako. Na Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Anayekadiria usiku na mchana na Anajua vipimo vyake na kipindi kinachopita na kusalia cha mchana na usiku. Mwenyezi Mungu Anajua kwamba haiwezekani kwenu nyinyi kusimama usiku wote, hivyo basi akawafanyia mambo kuwa mepesi kwenu. Na msome kwenye Swala ya usiku kile kilichokuwa chepesi kwenu kukisoma katika Qur’ani. Mwenyezi Mungu anajua kuwa miongoni mwenu kuna wanaoelemewa na ugonjwa wasiweze kusimama usiku. Na kuna watu wengine wanatembea ardhini kwa biashara na kazi wakitafuata riziki ya Mwenyezi Mungu ya halali. Na kuna watu wengine wanapigana jihadi katika njia ya Mwenye kuliinua neno Lake na kutangaza dini Yake. Basi someni kutoka kwenye Qur’ani kile kilicho chepesi kwenu, na endeleeni kutekeleza faradhi za Swala, na toeni Zaka za lazima kwenu, na toeni sadaka za mali yenu katika njia za wema na hisani kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu. Na chochote kile mnachokifanya miongoni mwa njia za wema na kheri na matendo ya utiifu, mtapata malipo yake na thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, hali ya kuwa ni bora zaidi kuliko kile mlichokitanguliza duniani na ni chenye thawabu kubwa zaidi. Na mtake msamaha wa Mwenyezi Mungu katika hali zenu zote. Hakika Mwenyezi Mumngu ni Msamehefu sana kwenu ni Mwenye huruma na nyinyi