Back to Languages

Swahili - Chapter 74 - Al-Muddaththir

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Muddaththir 74:1

Ewe uliojifinika nguo zako

Verse 2 — Surah Al-Muddaththir 74:2

Inuka kutoka kwenye malazi yako owaonye watu adhabu ya Menyezi Mungu

Verse 3 — Surah Al-Muddaththir 74:3

Na umkusudie Mola wako, Peke Yake, kwa kumtukuza, kumpwekesha na kumuabudu

Verse 4 — Surah Al-Muddaththir 74:4

Na usafishe nguo zako kutokana na najisi, kwani usafi wa nje ni katika kutimia usafi wa ndani

Verse 5 — Surah Al-Muddaththir 74:5

Na uendelee daima kuyaepuka masanamu na mizimu, na matendo ya ushirikina yote usiyakaribie

Verse 6 — Surah Al-Muddaththir 74:6

Na usitoe kitu kumpa mtu kwa lengo la kupata zaidi ya hiko. Na kwa ajili ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu

Verse 7 — Surah Al-Muddaththir 74:7

vumilia juu ya maamrisho na makatazo

Verse 8 — Surah Al-Muddaththir 74:8

Pindi patakapopulizwa kwenye barugumu mpulizo wa Ufufuzi na Uenezaji

Verse 9 — Surah Al-Muddaththir 74:9

wakati huo ni wakati ambao ni mgumu kwa makafiri

Verse 10 — Surah Al-Muddaththir 74:10

si rahisi kwao kusalimika na yale walionayo ya kujadiliwa hesabu zao na vituko vingine vikubwa

Verse 11 — Surah Al-Muddaththir 74:11

Niache mimi, ewe Mtume, na huyu niliyemuumba ndani ya tumbo la mamake akiwa peke yake, hana mali wala watoto

Verse 12 — Surah Al-Muddaththir 74:12

Nikamfanya awe na mali mengi yenye kuenea na watoto waliyoko na yeye hapo Makkah hawamuondokei. Na

Verse 13 — Surah Al-Muddaththir 74:13

nikamsahilishia kwa kumrahisishia njia za maisha. Kisha yeye anatarajia, baada ya vitu hivi alivyopewa

Verse 14 — Surah Al-Muddaththir 74:14

nimuongezee kwenye mali yake na watoto wake na huku yeye amenikanusha. Mambo sivyo kama anavyodai huyu mwenye kuasi, mtenda dhambi

Verse 15 — Surah Al-Muddaththir 74:15

Simuongezei zaidi ya hiko nilichompa

Verse 16 — Surah Al-Muddaththir 74:16

kwa kuwa yeye alikuwa mshindani mkanushaji wa Qur’ani na hoja za Mwenyezi Mungu kwa viumbe Wake

Verse 17 — Surah Al-Muddaththir 74:17

Nitambebesha mateso magumu na usumbufu usio na mapumziko. Anayekusudiwa hapa ni Al-Walid mwana wa Al-Mughi rah aliyekuwa akishindana na haki na akijitokeza kupigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Haya ndiyo malipo ya kila mwenye kushindana na haki na kuipiga vita

Verse 18 — Surah Al-Muddaththir 74:18

Kwa kweli yeye aliwaza ndani ya nafsi yake akatayarisha la kusema kumtukana Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani

Verse 19 — Surah Al-Muddaththir 74:19

Hivyo basi akalaaniwa na akastahili, kwa hilo, maangamivu: alijiandaa vipi ndani ya nafsi yake kwa hayo matukano

Verse 20 — Surah Al-Muddaththir 74:20

Kisha pia akalaaniwa

Verse 21 — Surah Al-Muddaththir 74:21

Kisha yeye alifikiria kuhusu kile alichokipanga na kukitayarisha cha kuitia dosari Qur’ani

Verse 22 — Surah Al-Muddaththir 74:22

Kisha akafinya uso wake na akazidi katika hali ile ya ukunjaji uso kwa kukosa hila za kufanya na kutopata ila yoyote ya kuitia dosari Qur’ani

Verse 23 — Surah Al-Muddaththir 74:23

Kisha akarudi kuipa mgongo haki na akajiona ni mkubwa wa kutofaa kuikubali

Verse 24 — Surah Al-Muddaththir 74:24

hapo akasema kuhusu Qur’ani, «Haya anayoyasema Muhammad si chochote isipokuwa ni uchawi uliopokewa kutoka kwa watu wa mwanzo waliopita

Verse 25 — Surah Al-Muddaththir 74:25

Haikuwa hi Qur’ani isipokuwa ni maneno ya viumbe ambayo Muhammad amejifunza kutoka kwao kisha akadai kuwa yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.»

Verse 26 — Surah Al-Muddaththir 74:26

Basi nitamuingiza kwenye moto wa Jahanamu ili alionje joto lake na achomeke kwa moto wake

Verse 27 — Surah Al-Muddaththir 74:27

Na ni lipi lililokujulisha wewe ni kitu gani hiyo Jahanamu

Verse 28 — Surah Al-Muddaththir 74:28

Haibakishi nyama wala haiachi mfupa isipokuwa huvichoma

Verse 29 — Surah Al-Muddaththir 74:29

Unageuza ngozi ya mwili, unazifanya ngozi kuwa nyeusi na unazichoma

Verse 30 — Surah Al-Muddaththir 74:30

Wanasimamia mambo yake na kushikilia kazi ya kuwatesa watu wake Malaika kumi na tisa katika washika zamu wa Motoni wenye nguvu

Verse 31 — Surah Al-Muddaththir 74:31

Na hatukuwafanya washika hazina wa Motoni isipokuwa miongoni mwa Malaika washupavu. Na hatukuiweka idadi hiyo isipokuwa kuwatahini wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na ili imani ya yakini ipatikane kwa wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu kwamba yaliyokuja ndani ya Qur’ani juu ya washika hazina wa Motoni ni ukweli utokao kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kwani hayo yanaafikiana na vitabu vyao, na ili Waumini wazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na waifuate Sheria Yake kivitendo, na ili wasilifanyie shaka hilo wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu wala wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ili wapate kusema wale wenye unafiki ndani ya nyoyo zao na makafiri, «Ni lipi alilolikusudia Mwenyezi Mungu kwa idadi hii ya ajabu?» Kwa mfano wa hayo yaliyotajwa, Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayetaka kumpoteza na Anamuongoza Anayetaka kumuongoza. Na hakuna ajuwaye idadi ya askari wa Mola wako, na miongoni mwao ni Malaika, isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na haukuwa huu Moto isipokuwa ni ukumbusho na mazingatio kwa watu

Verse 32 — Surah Al-Muddaththir 74:32

Mambo sivyo kama walivyotaja ya ukanushaji Mtume katika yale aliyokuja nayo! Anaapa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, kwa mwezi

Verse 33 — Surah Al-Muddaththir 74:33

na kwa usiku unapogeuka kwenda zake

Verse 34 — Surah Al-Muddaththir 74:34

na kwa asubuhi inapotoa mwangaza na kufunuka

Verse 35 — Surah Al-Muddaththir 74:35

hakika Moto ni mojawapo ya mambo makubwa

Verse 36 — Surah Al-Muddaththir 74:36

kwa ajili ya kuwaonya na kuwatisha watu

Verse 37 — Surah Al-Muddaththir 74:37

kwa anayetaka miongoni mwenu kujiweka karibu na Mola wake kwa kufanya matendo ya utiifu, au kujikalisha nyuma kwa kufanya matendo ya uasi

Verse 38 — Surah Al-Muddaththir 74:38

Kila nafsi imefungwa na kuwekwa rahani kwa ilichokitenda, miongoni mwa matendo mema au mabaya, kwa kukichuma. Haifunguliwi mpaka itekeleze haki zilizo juu ya lazima yake na ipatiwe mateso yanayostahili kupatiwa

Verse 39 — Surah Al-Muddaththir 74:39

Isipokuwa Waislamu waliotakaswa, watu wa upande wa kulia waliojikomboa shingo zao kwa utiifu

Verse 40 — Surah Al-Muddaththir 74:40

Wao watakuwa kwenye mabustani ya Peponi ambayo sifa zake hazifikiwi ukomo. Watakuwa wakiulizana wao kwa wao

Verse 41 — Surah Al-Muddaththir 74:41

kuhusu makafiri waliojikosea nafsi zao

Verse 42 — Surah Al-Muddaththir 74:42

«Ni lipi lililowaingiza kwenye moto wa Jahanamu na likawafanya

Verse 43 — Surah Al-Muddaththir 74:43

mlionje joto lake lililo kali sana?» Wahalifu waseme , «Hatukuwa ni miongoni mwa wanaoswali duniani

Verse 44 — Surah Al-Muddaththir 74:44

na hatukuwa tukitoa sadaka na kuwafanyia wema wahitaji na maskini

Verse 45 — Surah Al-Muddaththir 74:45

na tulikuwa tukizungumza maneno ya ubatilifu na watu wa upotofu na upotevu

Verse 46 — Surah Al-Muddaththir 74:46

na tulikuwa tukiikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa

Verse 47 — Surah Al-Muddaththir 74:47

mpaka kifo kikatujia na hali sisi tuko kwenye mambo hayo mabaya ya upotevu

Verse 48 — Surah Al-Muddaththir 74:48

Basi hayatawafalia neno maombezi ya wenye kuombea wote, miongoni mwa Malaika, Manabii na wengineo, kwa kuwa aombewaye ni yule aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na akamuidhinisha mwenye kumuombea

Verse 49 — Surah Al-Muddaththir 74:49

Basi wana nini hawa washirikina wamejiepusha na Qur’ani na

Verse 50 — Surah Al-Muddaththir 74:50

mawaidha yaliyomo ndani yake? Kama kwamba wao ni pundamilia wanaobabaika

Verse 51 — Surah Al-Muddaththir 74:51

wanaomkimbia simba mshambulizi

Verse 52 — Surah Al-Muddaththir 74:52

Lakini kila mmoja, miongoni mwa hawa washirikina, ana matumaini ateremshiwe kitabu kutoka mbinguni kilichokunjuliwa kama kile kilichoteremshiwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

Verse 53 — Surah Al-Muddaththir 74:53

Mambo si hivyo kama wanavyodai. Ukweli ni kwamba wao hawaiogopi Akhera wala hawaamini kuwa kuna kufufuliwa na kulipwa

Verse 54 — Surah Al-Muddaththir 74:54

Ni kweli kwamba Qur’ani ni mawaidha yenye ufasaha, yanayotosha kuwafanya wao wawaidhike

Verse 55 — Surah Al-Muddaththir 74:55

Anayetaka kuwaidhika, basi na awaidhike kwa yaliyomo ndani yake na anufaike na uongofu wake

Verse 56 — Surah Al-Muddaththir 74:56

Na hawawaidhiki kwayo isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Amewatakia kuongoka. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayestahiki kuogopewa na kutiiwa, na Ndiye Anayestahiki kumsamehe anayemuamini Yeye na kumtii