Back to Languages

Swahili - Chapter 75 - Al-Qiyamah

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Qiyamah 75:1

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Hesabu na Malipo

Verse 2 — Surah Al-Qiyamah 75:2

na Anaapa kwa nafsi yenye kuamini na kuchamungu, inayomlaumu mwenyewe kwa kuacha matendo ya utiifu na kufanya matendo yenye kuangamiza, kwamba watu watafufuliwa

Verse 3 — Surah Al-Qiyamah 75:3

Je anadhanihuyu binadamu kafiri kuwa sisi hatutaweza kuikusanya mifupa yake baada ya kuwa mbalimbali

Verse 4 — Surah Al-Qiyamah 75:4

Ndio! Tutaikusanya na tunaweza kufanya vidole vyake au ncha za vidole vyake- baada ya kuvikusanya na kuzioanisha- viwe kwenye umbo la sawasawa, kama vilivyokuwa kabla ya kufa

Verse 5 — Surah Al-Qiyamah 75:5

Bali binadamu anakanusha kufufuliwa, anataka asalie kwenye kufanya ubaya kwa siku za mbeleni za maisha yake

Verse 6 — Surah Al-Qiyamah 75:6

Kafiri huyu huwa akiuliza, akiliona jambo la kusimama Kiyama kuwa liko mbali, «Ni lini Siku ya Kiyama?’

Verse 7 — Surah Al-Qiyamah 75:7

Basi macho yatakapoduwaa na yakashituka kwa kutishika na kile yalichokiona cha vituko vya Siku ya Kiyama

Verse 8 — Surah Al-Qiyamah 75:8

na ukafutika mwangaza wa mwezi

Verse 9 — Surah Al-Qiyamah 75:9

na vikakusanywa jua na mwezi katika kukosa mwangaza, kikawa kila mojawapo ya hivyo viwili hakina mwangaza

Verse 10 — Surah Al-Qiyamah 75:10

wakati huo binadamu atasema, «Pa kukimbilia ni wapi kuiepuka adhabu?»

Verse 11 — Surah Al-Qiyamah 75:11

Mambo sivyo kama unavyotamani yawe, ewe binadamu, ya kutaka kukimbia. Huna mahali pa kukimbilia wala pa kupata uokozinfsi yake

Verse 12 — Surah Al-Qiyamah 75:12

Kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake ndio mwisho wa viumbe Siku ya Kiyama na ndipo mahali pao pa kutulia, na hapo Amlipe kila mtu kwa kile alichostahiki

Verse 13 — Surah Al-Qiyamah 75:13

Atapashwa habari binadamu Siku hiyo kwa matendo yake yote, mema na mabaya, aliyoyatanguliza miongoni mwa hayo katika maisha yake na aliyoyachelewesha

Verse 14 — Surah Al-Qiyamah 75:14

Bali binadamu ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake, yenye kumfuata kwa alichokitenda na alichokiacha

Verse 15 — Surah Al-Qiyamah 75:15

hata kama atakuja na kila udhuru wa kuelezea sababu ya uhalifu wake, hilo halitamfaa

Verse 16 — Surah Al-Qiyamah 75:16

Usitikise, ewe Nabii, ulimi wako kwa Qur’ani wakati wahyi unapoteremka ili ufanye haraka kuihifadhi kwa kuogopa isikuponyoke

Verse 17 — Surah Al-Qiyamah 75:17

Kwani ni juu yetu sisi kuikusanya kwenye kifua chako kisha uisome kwa ulimi wako wakati utakapo. Mjumbe wetu Jibrili akikusomea

Verse 18 — Surah Al-Qiyamah 75:18

basi kisikilize kisomo chake na umpulikize. Kisha isome kama alivyokusomea

Verse 19 — Surah Al-Qiyamah 75:19

kisha ni juu yetu kukuelezea kilichokutatiza kukifahamu katika maana yake na hukumu zake

Verse 20 — Surah Al-Qiyamah 75:20

Mambo sivyo kama mlivyodai, enyi mkusanyiko wa washirikina, kuwa hakuna kufufuliwa wala kulipwa

Verse 21 — Surah Al-Qiyamah 75:21

Bali nyinyi ni watu mnaopenda dunia na pambo lake na mnaacha Akhera na starehe zake

Verse 22 — Surah Al-Qiyamah 75:22

Nyuso za watu wema Siku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kung’ara, nzuri na zenye furaha

Verse 23 — Surah Al-Qiyamah 75:23

zitamuona Mola Aliyeziumba na Anayezimiliki, na zitastarehe kwa hilo

Verse 24 — Surah Al-Qiyamah 75:24

Nyuso za watu wabaya Silku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kukunjana na kusinyaa

Verse 25 — Surah Al-Qiyamah 75:25

zinatazamia kushukiwa na msiba mkubwa wenye kuvunja

Verse 26 — Surah Al-Qiyamah 75:26

Ni kweli! Pindi roho itakapofika sehemu za juu za kifua

Verse 27 — Surah Al-Qiyamah 75:27

na wakasema baadhi ya waliohudhuria kuwaambia wengine, «Je kuna mtu wa kumzungua na kumpoza kutokana na hali hii aliyonayo?»

Verse 28 — Surah Al-Qiyamah 75:28

Na yule ambaye yuko katika hali ya kufa akajua kwamba lile lililomshukia ni kuaga dunia, kwa kuwa anawaona Malaika wa mauti

Verse 29 — Surah Al-Qiyamah 75:29

Na ikashikana shida ya mwisho wa duniani na shida ya mwanzo wa Akhera. Kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka

Verse 30 — Surah Al-Qiyamah 75:30

Watu watapelekwa Siku ya Kiyama: ima Peponi au Motoni

Verse 31 — Surah Al-Qiyamah 75:31

Hakuwa kafiri ni mwenye kumuamini Mtume na Qur’ani, wala hakuwa ni mwenye kumtekelezea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Swala za faradhi

Verse 32 — Surah Al-Qiyamah 75:32

Lakini aliikanusha Qur’ani na akaipa mgongo Imani

Verse 33 — Surah Al-Qiyamah 75:33

kisha akaenda kwa watu wake akijiona hali ya kujigamba katika kutembea kwake. Basi maangamivu

Verse 34 — Surah Al-Qiyamah 75:34

ni yako baada ya maangamivu

Verse 35 — Surah Al-Qiyamah 75:35

Kisha maangamivu ni yako baada ya maangamivu

Verse 36 — Surah Al-Qiyamah 75:36

Je anadhani huyu binadamu anayekanusha kufufuliwa kuwa ataachwa bure: haamrishwi wala hakatazwi, hahesabiwi wala hateswi

Verse 37 — Surah Al-Qiyamah 75:37

Kwani hakuwa binadamu huyu ni tone la manii dhaifu linalotokana na maji matwevu yanayomwagwa na kumiminwa kwenye kizazi

Verse 38 — Surah Al-Qiyamah 75:38

kisha yakawa ni kipande cha damu iliyo kavu. Mwenyezi Mungu Akaliumba kwa uweza Wake na Akazilinganisha sura zake katika umbo la mwili lililo zuri kabisa

Verse 39 — Surah Al-Qiyamah 75:39

Akafanya kutokana na binadamu huyu jinsi mbili: ya kiume na ya kike. Je kwani hakuwa Mola huyo Muumba wa vitu hivyo ni Muweza wa kuwarudisha viumbe wakiwa hai baada ya kutoweka kwao

Verse 40 — Surah Al-Qiyamah 75:40

Ndio! Anaweza. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hakika ni Muweza wa hilo