Back to Languages

Swahili - Chapter 77 - Al-Mursalat

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Mursalat 77:1

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa upepo unapovuma kwa mfululizo, huu baada ya huu

Verse 2 — Surah Al-Mursalat 77:2

Na kwa upepo wenye kuvuma kwa ukali wenye kuangamiza

Verse 3 — Surah Al-Mursalat 77:3

Na kwa Malaika waliopewa jukumu la mawingu, wakawa wayapeleka pale anapotaka Mwenyezi Mungu

Verse 4 — Surah Al-Mursalat 77:4

Na kwa Malaika wanaoshuka, kutoka kwa Mwenyezi Mungu

Verse 5 — Surah Al-Mursalat 77:5

na amri zinazopambanua baina ya haki na batili na halali na haramu

Verse 6 — Surah Al-Mursalat 77:6

Na kwa Malaika wanaoupokea wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuuteremsha kwa Manabii Wake, unaowapa viumbe wake udhuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na pia onyo kutoka Kwake, ili watu wasiwe na hoja

Verse 7 — Surah Al-Mursalat 77:7

Hakika jambo la Kiyama mnaloahidiwa pamoja na lile la kuhesabiwa na kulipwa ni lenye kuwa hapana shaka

Verse 8 — Surah Al-Mursalat 77:8

Basi nyota zitakapofutwa na mwangaza wake ukaondoka

Verse 9 — Surah Al-Mursalat 77:9

na mbingu zitakapopasuka

Verse 10 — Surah Al-Mursalat 77:10

na majabali yatakapopeperuka na kukueanea huku na kule na yakawa ni mapepe yanayorushwa na upepo

Verse 11 — Surah Al-Mursalat 77:11

Na Mitume watapowekewa wakati na muda wa baina yao na ummah wao na kusemwe

Verse 12 — Surah Al-Mursalat 77:12

«Ni Siku kubwa gani Mitume wameahirishiwa?»

Verse 13 — Surah Al-Mursalat 77:13

Wameahirishiwa Siku ya hukumu na uamuzi baina ya viumbe

Verse 14 — Surah Al-Mursalat 77:14

Na nilipi lililokujulisha wewe, ewe binadamu, ni siku gani hiyo ya kutolewa uamuzi na ni zipi shida zake na vituko vyake

Verse 15 — Surah Al-Mursalat 77:15

Maangamivu makubwa Siku hiyo ni ya wale waliyoikanusha Siku hii iliyoahidiwa

Verse 16 — Surah Al-Mursalat 77:16

Kwani hatukuawaangamiza walitangulia kati ya umma waliopita kwa kuwakanusha kwao Mitume, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd

Verse 17 — Surah Al-Mursalat 77:17

Kisha tutawakutanisha na wao wale waliokuja nyuma kati ya wale waliokuwa ni kama wao katika ukanushaji na uasi

Verse 18 — Surah Al-Mursalat 77:18

Mfano wa uangamizaji huo mkali ndivyo tutakavyowafanya wahalifu kati ya makafiri wa Makkah, kwa kumkanusha kwao Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

Verse 19 — Surah Al-Mursalat 77:19

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa kila mwenye kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, unabii, kufufuliwa na kuhesabiwa

Verse 20 — Surah Al-Mursalat 77:20

Je kwani sisi hatukuwaumba nyinyi, enyi mkusanyiko wa makafiri, kutokana na maji dhaifu yaliyo matwevu nayo ni tone la manii

Verse 21 — Surah Al-Mursalat 77:21

tukayaweka maji haya kwenye mahali palipohifadhika, napo ni kizazi cha mwanamke

Verse 22 — Surah Al-Mursalat 77:22

mpaka kipindi maalumu kinachojulikana na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

Verse 23 — Surah Al-Mursalat 77:23

Tukaweza kumuumba, kumtia sura na kumtoa. Basi bora wa wenye kuweza ni s isi

Verse 24 — Surah Al-Mursalat 77:24

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kukanusha uweza wetu

Verse 25 — Surah Al-Mursalat 77:25

Je kwani hatukuifanya hii ardhi mnayoishi juu yake

Verse 26 — Surah Al-Mursalat 77:26

ikusanye juu ya mgongo wake walio hai wasiohesabika, na ndani ya matumbo yake wafu wasiodhibitika, na

Verse 27 — Surah Al-Mursalat 77:27

tukajaalia iwe na majabali yaliyojikita yaliyo marefu ili isitikisike na nyinyi, na tukawanywesha maji tamu yaliyo mazuri

Verse 28 — Surah Al-Mursalat 77:28

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa waliozikanusha neema hizi

Verse 29 — Surah Al-Mursalat 77:29

Wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama, «Endeni kwenye adhabu ya moto wa Jahanamu mliokuwa mkiukanusha duniani

Verse 30 — Surah Al-Mursalat 77:30

Endeni mjifinike kwenye kivuli cha moshi wa moto wa Jahanamu ambacho hapo panachembuka vipande vitatu

Verse 31 — Surah Al-Mursalat 77:31

Kivuli hiko hakimfanyi mtu ahifadhike na joto la Siku hiyo wala hakizuii muwako wa Moto chochote

Verse 32 — Surah Al-Mursalat 77:32

Hakika moto wa Jahanamu unarusha macheche makubwa ya moto, kila cheche moja katika hayo ni kama jengo lililoimarishwa katika ukubwa na urefu wa kuenda juu

Verse 33 — Surah Al-Mursalat 77:33

Kama kwamba hizo cheche za moto wa Jahanamu zinazopaa juu ni ngamia weusi ambao rangi yao imeingia kwenye umanjano.»

Verse 34 — Surah Al-Mursalat 77:34

Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kukanusha mateso yaliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu

Verse 35 — Surah Al-Mursalat 77:35

Hii ndiyo Siku ya Kiyama ambayo wakanushaji hawatatamka maneno ya kuwanufaisha

Verse 36 — Surah Al-Mursalat 77:36

wala hawatapewa idhini ya kusema wakatoa nyudhuru, kwa kuwa hawatakuwa na udhuru wowote

Verse 37 — Surah Al-Mursalat 77:37

Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kuikanusha siku hii na yaliyomo ndani yake

Verse 38 — Surah Al-Mursalat 77:38

Hii ni Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atatoa uamuzi baina ya viumbe, na ukweli na ubatilifu utapambanuka. Tutawakusanya nyinyi Siku hiyo, enyi makafiri wa ummah huu, pamoja na makafiri wa mwanzo miongoni mwa ummah waliopita

Verse 39 — Surah Al-Mursalat 77:39

Basi mkiwa na hila za kujitoa na adhabu, tumieni hila zenu na mziokoe nafsi zenu na msukosuko wa Mwenyezi Mungu na mateso Yake

Verse 40 — Surah Al-Mursalat 77:40

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Kiyama

Verse 41 — Surah Al-Mursalat 77:41

Hakika ya wale waliomuogopa Mola wao duniani na wakaiogopa adhabu Yake kwa kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Wao Siku ya Kiyama watakuwa kwenye vivuli vya miti vilivyonyoka, na chemchemi za maji zinazotembea

Verse 42 — Surah Al-Mursalat 77:42

na matunda mengi yanayopendwa na nafsi zao ambayo wao wanastarehe nayo. Hapo waambiwe

Verse 43 — Surah Al-Mursalat 77:43

«Kuleni chakula chenye ladha na mnyweni kinywaji chenye kufurahisha kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza duniani.»

Verse 44 — Surah Al-Mursalat 77:44

Sisi, kwa mfano wa malipo hayo makubwa, tutawalipa watu wema katika matendo yao na utiifu wao kwetu

Verse 45 — Surah Al-Mursalat 77:45

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Malipo na Hesabu, na kuzikanusha sterehe na mateso yaliyomo Siku hiyo

Verse 46 — Surah Al-Mursalat 77:46

Kisha Mwenyezi Mungu Akawaonya makafiri kwa kusema, «Kuleni aina ya vyakula vya ladha duniani na stareheni kwa matamanio yake yenye kumalizika kwa muda mchache, hakika nyinyi ni wahalifu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.»

Verse 47 — Surah Al-Mursalat 77:47

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa

Verse 48 — Surah Al-Mursalat 77:48

Na wanapoambiwa hawa washirikina, «Mswalieni Mwenyezi Mungu na mnyenyekeeni,» hawanyenyekei wala hawaswali, bali wanaendelea kuonyesha kiburi chao

Verse 49 — Surah Al-Mursalat 77:49

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu

Verse 50 — Surah Al-Mursalat 77:50

Iwapo wao hawataiamini hii Qur’ani, basi wataamini kitabu gani na maneno gani baada yake? Na Qur’ani yenyewe ni Kitabu kilichobainisha kila kitu, kilicho wazi katika hekima zake, hukumu zake na habari zake, chenye kushinda katika matamko yake na maana yake