Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 78 - An-Naba
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah An-Naba 78:1
Kuhusu kitu gani baadhi ya makafiri wa Kikureshi wanaulizana
Verse 2 — Surah An-Naba 78:2
Wanaulizana kuhusu habari iliyo na uzito mkubwa kabisa
Verse 3 — Surah An-Naba 78:3
nayo ni Qur’ani tukufu inayotoa habari za kufufuliwa ambako makafiri wa Kikureshi wana shaka nako na wanakukanusha
Verse 4 — Surah An-Naba 78:4
Mambo sivyo kama wanavyodhania hawa washirikina. Hapo watajua hawa washirikina upeo wa kukanusha kwao na kitawadhihirikia waziwazi kile Atakachowatenda Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama
Verse 5 — Surah An-Naba 78:5
Kisha litahakikishika kwao jambo hilo na utahakikishika kwao ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuhusu Qur’ani na kufufuliwa. Huu ni utisho na makemeo kwao
Verse 6 — Surah An-Naba 78:6
Kwani hatukuwatandazia ardhi kama tandiko
Verse 7 — Surah An-Naba 78:7
Na Tukawafanyia majabali kuwa ni vigingi, ili isitisike nanyi
Verse 8 — Surah An-Naba 78:8
Na Tukawaumba aina mbali-mbali, mume na mke
Verse 9 — Surah An-Naba 78:9
Na Tukafanya usingizi wenu ni mapumziko kwa viwiliwili vyenu: ndani yake mnatulia na kupumzika
Verse 10 — Surah An-Naba 78:10
Na Tukaufanya usiku kuwa ni vazi, unawavisha giza lake na kuwafinika, kama nguo inavyomsitiri mwenye kuivaa
Verse 11 — Surah An-Naba 78:11
Na Tukaufanya mchana ni kipindi cha kutafuta maisha, mnaenea humo kwa ajili ya maisha yenu na mnatembea humo kwa ajili ya maslahi yenu
Verse 12 — Surah An-Naba 78:12
Na Tukajenga juu yenu mbingu saba, madhubuti jengo lake, lilioumbwa kwa uzuri, halina mapasuko wala nyufa
Verse 13 — Surah An-Naba 78:13
Na Tukalifanya jua kuwa ni taa iwakayo na kung’ara
Verse 14 — Surah An-Naba 78:14
Na Tukateremsha kutoka kwenye mawingu yanyeshayo maji yamiminikayo kwa wingi
Verse 15 — Surah An-Naba 78:15
ili Tutoe kwa maji hayo nafaka inayoliwa na watu
Verse 16 — Surah An-Naba 78:16
nyasi zinazoliwa na wanyama na miti iliyosongamana kwa kutawanyika tagaa zake
Verse 17 — Surah An-Naba 78:17
Hakika Siku ya Uamuzi kati ya viumbe
Verse 18 — Surah An-Naba 78:18
nayo ni Siku ya Kiyama, imekuwa ni wakati na ahadi iliyowekewa muda maalimu kwa watu wa mwanzo na wa mwisho
Verse 19 — Surah An-Naba 78:19
Na zikafunguliwa mbingu zikawa ni zenye milango mingi kwa ajili ya kuteremka Malaika
Verse 20 — Surah An-Naba 78:20
Na yakalipuliwa majabali baada ya kuwa yamekita, yakawa ni kama mangati
Verse 21 — Surah An-Naba 78:21
Hakika Jahanamu, Siku Hiyo, itawalindiza wenye ukafiri ambao Moto huo umeandaliwa wao
Verse 22 — Surah An-Naba 78:22
Kwa makafiri ndio marejeo
Verse 23 — Surah An-Naba 78:23
Watabakia humo muda mrefu ufuatanao, usiokoma
Verse 24 — Surah An-Naba 78:24
Hawatakula humo chochote kitakachozizimisha joto la moto kwao
Verse 25 — Surah An-Naba 78:25
Wala kinywaji kitakachowaondolea kiu yao. Isipokuwa maji moto na usaha wa watu wa motoni
Verse 26 — Surah An-Naba 78:26
Watakuwa wanalipwa kwa hilo malipo ya sawa yanayolingana na vitendo vyao walivyovitenda duniani
Verse 27 — Surah An-Naba 78:27
Hakika wao walikuwa hawaiyogopi Siku ya Hesabu, na kwa hivyo hawakujitayarisha nayo kwa kufanya matendo ya kuwafaa
Verse 28 — Surah An-Naba 78:28
Na waliyakanusha waziwazi yaliyoletwa na Mitume
Verse 29 — Surah An-Naba 78:29
Na kila kitu Tulikijua na Tukakiandika katika Ubao uliohifadhiwa (Al-Lawḥ Al-Maḥfūd)
Verse 30 — Surah An-Naba 78:30
Basi Onjeni, enyi makafiri, hayo yakiwa ni malipo ya vitendo vyenu, Hatutawazidishia isipokuwa adhabu juu ya adhabu yenu
Verse 31 — Surah An-Naba 78:31
Hakika kwa wale ambao wanamuogopa Mola wao na huku wanatenda mema kuna kufaulu kwa kuingia Peponi
Verse 32 — Surah An-Naba 78:32
Hakika watapata Mabustani makubwa na zabibu
Verse 33 — Surah An-Naba 78:33
Na watapata wanawake wenye umri mdogo, wenye vifua vilivyojaza, marika na waume zao
Verse 34 — Surah An-Naba 78:34
Na watapata glasi zlizojaa pombe
Verse 35 — Surah An-Naba 78:35
Hawatasikia katika Pepo hiyo maneno ya upotofu wala kudanganyana
Verse 36 — Surah An-Naba 78:36
Watayapata yote hayo yakiwa ni malipo na zawadi na kipewa kingi cha kuwatosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu
Verse 37 — Surah An-Naba 78:37
Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati ya hizo, Mwenye kuwarehemu duniani na Akhera. Hawataweza kumuomba isipokuwa kile walichopewa ruhusa kumuomba
Verse 38 — Surah An-Naba 78:38
Siku atakaposimama Jibrili na Malaika wengine hali ya kujipanga mlolongo. Hawatamuombea isipokuwa yule aliyetolewa ruhusa na Mwingi wa Rehema ya kuombewa na akasema maneno ya haki na ya sawa
Verse 39 — Surah An-Naba 78:39
Hiyo ndiyo siku ya haki isiyokuwa na shaka kuja kwake. Kwa hivyo, yule atakaye kuokoka na vituko vya Siku hiyo, na ajifanyie njia ya marejeo kwa Mola wake kutenda vitendo vyema
Verse 40 — Surah An-Naba 78:40
Sisi Tunawaonya nyinyi adhabu ya Siku ya mwisho iliyo karibu. Siku ambayo atayaona kila mtu aliyoyatenda katika kheri au aliyoyachuma miongoni mwa madhambi. Na kafiri atasema, kwa kitisho cha Hesabu, «Laiti mimi nilikuwa mchanga na sikufufuliwa.»