Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 80 - Abasa
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah Abasa 80:1
Yalidhihiri mabadiliko na mkunjiko katika uso wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
Verse 2 — Surah Abasa 80:2
na akapa nyongo kwa sababu ya kwamba Abdallah bin Ummi Maktum alimjilia akitaka aelekezwe. Na alikuwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ameshughulika kuwalingania miamba wa Kikureshi katika Uislamu
Verse 3 — Surah Abasa 80:3
Ni kitu gani kinakufanya wewe ujue uhakika wa jambo lake? Kwani huenda ikawa, kwa kuuliza kwake, nafsi yake itatakasika na kusafika
Verse 4 — Surah Abasa 80:4
Au pengine apate mazingatio zaidi na kutishika
Verse 5 — Surah Abasa 80:5
Basi yule alijyejitosheleza na kutouhitajia uongozi wako
Verse 6 — Surah Abasa 80:6
wewe ndiye unayemjali na wapulikiza maneno yake
Verse 7 — Surah Abasa 80:7
Na ni kitu gani kinachokupa jukumu kwako iwapo hakusafika na ukafiri wake
Verse 8 — Surah Abasa 80:8
Ama yule ambaye amekuwa na pupa la kukutana na wewe
Verse 9 — Surah Abasa 80:9
na huku anamuogopa Mwenyezi Mungu asiwe na kasoro katika kupata uongofu
Verse 10 — Surah Abasa 80:10
wewe unampuuza. Ilivyotakikana ufanye si kama ulivyofanya, ewe Mtume
Verse 11 — Surah Abasa 80:11
Hakika Sura hii ni mawaidha kwako na kwa kila anayetaka kuwaidhika
Verse 12 — Surah Abasa 80:12
Basi atakaye atamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja na atafuata Wahyi Wake
Verse 13 — Surah Abasa 80:13
Wahyi huu, nao ni Qur’ani, uko katika kurasa zilizotukuzwa
Verse 14 — Surah Abasa 80:14
zenye kuheshimiwa, zenye cheo cha juu
Verse 15 — Surah Abasa 80:15
zilizosafishwa na uchafu, uongezaji na upunguzaji
Verse 16 — Surah Abasa 80:16
Zilizoko mikononi mwa Malaika waandishi, mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, wenye maumbile mema, tabia zao ni nzuri na njema na pia matendo yao
Verse 17 — Surah Abasa 80:17
Amelaaniwa mtu kafiri na ataadhibiwa. Ni uovu ulioje wa ukafiri wake kwa Mola wake
Verse 18 — Surah Abasa 80:18
Kwani hajui ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Alimuumba kwacho mwanzo wake
Verse 19 — Surah Abasa 80:19
Mwenyezi Mungu Alimuumba kwa maji machache, nayo ni manii. Akayakadiria miongo yake
Verse 20 — Surah Abasa 80:20
Kisha Akambainishia njia ya kheri na ya shari
Verse 21 — Surah Abasa 80:21
Kisha humkosesha uhai, na Amemuekea mahali pa kuzikiwa
Verse 22 — Surah Abasa 80:22
Kisha Akitaka Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa mbaya, Atamhuisha na kumfufua baada ya kifo chake, kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa
Verse 23 — Surah Abasa 80:23
Mambo siyo kama yale anayoyasema kafiri na anayoyafanya. Bado hajatakeleza Aliyomuamrisha kwayo Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda wema kwa kumtii
Verse 24 — Surah Abasa 80:24
Na azingatie binadamu, vipi Mwenyezi Mungu Amekiumba chakula chake ambacho ndicho kinachoendeleza maisha yake
Verse 25 — Surah Abasa 80:25
Aone kwamba Sisi Tumeyamimina maji ya mvua juu ya ardhi kwa wingi
Verse 26 — Surah Abasa 80:26
Kisha Tumeipasua ardhi kwa Tulivyo vitoa kutoka humo miongoni mwa mimea tofauti
Verse 27 — Surah Abasa 80:27
Tukaotesha humo nafaka
Verse 28 — Surah Abasa 80:28
na zabibu, na nyasi za wanyama.Na mizaituni na mitende
Verse 29 — Surah Abasa 80:29
Na mabustani yenye miti mikubwa
Verse 30 — Surah Abasa 80:30
Na matunda
Verse 31 — Surah Abasa 80:31
na ndisha
Verse 32 — Surah Abasa 80:32
Mnajistareheshea kwazo, nyinyi na wanyama wenu
Verse 33 — Surah Abasa 80:33
Utakapokuja Ukelele wa Siku ya Kiyama, ambao utayatia uziwi, kwa kitisho chake, masikizi
Verse 34 — Surah Abasa 80:34
Siku mtu atakapomkimbia, kwa kitisho cha Siku Hiyo, nduguye
Verse 35 — Surah Abasa 80:35
na babake na mamake na
Verse 36 — Surah Abasa 80:36
mkewe na wanawe
Verse 37 — Surah Abasa 80:37
Kila mmoja Siku Hiyo, atakuwa na jambo litakalomzuia asishughulike na mwingine
Verse 38 — Surah Abasa 80:38
Nyuso za wenye neema, Siku Hiyo, zitakuwa ni zenye kung’ara
Verse 39 — Surah Abasa 80:39
zenye furaha na nderemo
Verse 40 — Surah Abasa 80:40
Na nyuso za watu wa Motoni zitakuwa na giza
Verse 41 — Surah Abasa 80:41
nyeusi, zafinikwa na unyonge
Verse 42 — Surah Abasa 80:42
Hao wenye kusifika na sifa hiyo ndiwo wale waliozikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wakazikanusha aya zake na wakayakeuka Aliyoyaharamisha kwa kutenda maovu na kukiuka mipaka