Back to Languages

Swahili - Chapter 82 - Al-Infitar

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Infitar 82:1

Pindi mbingu zitakapopasuka na ukaharibika mpango wake

Verse 2 — Surah Al-Infitar 82:2

Na pindi nyota zitakapoangukiana

Verse 3 — Surah Al-Infitar 82:3

Na pindi Mwenyezi Mungu Atakapozifanya bahari kulipuka na maji yake kutoweka

Verse 4 — Surah Al-Infitar 82:4

Na pindi makaburi yatakapogeuzwa kwa kufufuliwa waliokuwamo ndani yake

Verse 5 — Surah Al-Infitar 82:5

Wakati huo itajua kila nafsi vitendo vyake vyote ilivyovifanya, vilivyotangulia na vilivyoahirika na italipwa kwa vitendo hivyo

Verse 6 — Surah Al-Infitar 82:6

Ewe binadamu unayekanusha kufufuliwa! Ni kipi kilichokufanya uhadaike na ughurike kuhusu Mola wako Mpaji Mwenye kheri nyingi, Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa

Verse 7 — Surah Al-Infitar 82:7

Kwani si Yeye Aliyekuumba, Akalisawazisha umbo lako, Akakuweka katika hali ya sawa na Akakurekibisha ili uweze kutekeleza nyadhifa zako

Verse 8 — Surah Al-Infitar 82:8

katika sura yoyote ile Aliyoitaka Akakuumba

Verse 9 — Surah Al-Infitar 82:9

Mambo hayako kama vile mnavyosema kwamba nyinyi mna haki ya kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Hesabu na Malipo

Verse 10 — Surah Al-Infitar 82:10

Na mjue kuwa wako na nyinyi Malaika wachunguzi

Verse 11 — Surah Al-Infitar 82:11

watukufu kwa Mwenyezi Mungu, waandishi wa yale waliyowakilishwa kuyadhibiti. Hakiwapiti, katika vitendo vyenu na siri zenu, chochote

Verse 12 — Surah Al-Infitar 82:12

Wanayajua mnayoyafanya, ya kheri au ya shari

Verse 13 — Surah Al-Infitar 82:13

Hakika wachamungu wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa kwenye neema

Verse 14 — Surah Al-Infitar 82:14

Hakika watu waovu waliopuuza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa katika Moto mkali

Verse 15 — Surah Al-Infitar 82:15

Ukali wake, Moto huo, utawapata Siku ya Malipo.Na wala wao hawatakuwa ni wenye kughibu

Verse 16 — Surah Al-Infitar 82:16

wakawa hawamo ndani ya Moto wa Jahanamu, si kwa kutoka wala kwa kufa

Verse 17 — Surah Al-Infitar 82:17

Ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu

Verse 18 — Surah Al-Infitar 82:18

Kisha ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu

Verse 19 — Surah Al-Infitar 82:19

Siku ya Hesabu, hataweza yoyote kumnufaisha yoyote. Na amri zote Siku Hiyo ni za Mwenyezi Mungu Peke yake Ambaye hakuna mwenye kumshinda, wala hakuna mwenye kumtendesha nguvu, wala hakuna mwenye kushindana na Yeye