Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 86 - At-Tariq
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah At-Tariq 86:1
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu na nyota yenye kuchomoza usiku
Verse 2 — Surah At-Tariq 86:2
Na ni lipi lilokujulisha ni ukubwa gani wa nyota hiyo
Verse 3 — Surah At-Tariq 86:3
Hiyo ni nyota ing’arao na kuzagaa
Verse 4 — Surah At-Tariq 86:4
Hakuna nafsi yoyote isipokuwa amewakilishwa kwayo Malaika mwenye kuchunguza na kusjili amali zake ili ihesabiwe Siku ya Kiyama
Verse 5 — Surah At-Tariq 86:5
Basi aangalie binadamu mwenye kukanusha kufufuliwa ameumbwa kwa kitu gani? Ili ajue kuwa kurudisha umbo lake mara ya pili si vigumu kama kuumbwa mara ya kwanza
Verse 6 — Surah At-Tariq 86:6
Aliumbwa kwa manii yenye kupenyeza ndani ya uzao kwa haraka
Verse 7 — Surah At-Tariq 86:7
Yatokayo kwenye mgongo wa mwnamume na kifua cha mwanamke
Verse 8 — Surah At-Tariq 86:8
Hakika yule Aliyemuumba binadamu kwa maji haya ni muweza wa kumrudisha kwenye uhai baada ya kufa
Verse 9 — Surah At-Tariq 86:9
Siku zitakapofunuliwa wazi siri ziliofichwa na nafsi na kupambanuliwa njema na mbovu
Verse 10 — Surah At-Tariq 86:10
Binadamu hatakuwa na nguvu ya kuitetea nafsi yake wala hatakuwa na mtetezi wa kumwepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu
Verse 11 — Surah At-Tariq 86:11
Na Anaapa kwa mbingu yenye mvua ya kukaririka
Verse 12 — Surah At-Tariq 86:12
Na ardhi yenye pasuko za kufanya mimea ichipuke
Verse 13 — Surah At-Tariq 86:13
Hakika Qur’ani ni neno lenye kupambanua baina ya haki na batili
Verse 14 — Surah At-Tariq 86:14
Na si upuuzi. Haifai kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Akifanya hivyo atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu
Verse 15 — Surah At-Tariq 86:15
Hakika wenye kumkanusha Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani wanafanya vitimbi na mipango ili kuipinga haki na kuitilia nguvu batili
Verse 16 — Surah At-Tariq 86:16
Na Mimi nafanya vitimbi kuidhihirisha haki ingawa makafiri wanatukia.Usiwe na haraka nao, ewe Mtume, kutaka wateremshiwe adhabu
Verse 17 — Surah At-Tariq 86:17
Wape muhula uwangojee muda mchache wala usiwafanyie haraka, utaona adhabu itakayowafikia, mateso na maangamivu