Back to Languages

Swahili - Chapter 87 - Al-Ala

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Ala 87:1

Takasa Jina la Mola wako Aliyetukuka na kuepukana na mshirika na kila sifa pungufu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na utakatifu Wake

Verse 2 — Surah Al-Ala 87:2

Aliyeumba viumbe Akalitengeneza umbo lao na kulifanya zuri

Verse 3 — Surah Al-Ala 87:3

Na Aliyekadiria kila kitu na kukipeleka njia inayonasibiana nacho

Verse 4 — Surah Al-Ala 87:4

Na Aliyeotesha nyasi mbiti zenye rangi ya kijani

Verse 5 — Surah Al-Ala 87:5

Akazifanya baadaye kuwa kavu zilizobadilika rangi

Verse 6 — Surah Al-Ala 87:6

Tutakusomea, ewe Mtume, hii Qur’ani kisomo ambacho hutakisahau

Verse 7 — Surah Al-Ala 87:7

Isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Ataka usahau kwa hekima na maslahi anayoyajua Yeye. Kwani Yeye ni Mjuzi wa yaliyo wazi na yaliyofichika, ya maneno na ya vitendo

Verse 8 — Surah Al-Ala 87:8

Tutakufanyia mapesi mambo yako yote; miongoni mwayo ni kukusahilishia kubeba majukumu ya utume na kuifanya nyepesi Dini uliyokuja nayo

Verse 9 — Surah Al-Ala 87:9

Basi wawaidhie kaumu zako, ewe Mtume, kwa namna tulivyokutayarishia ufanye kwenye wahyi ulioletewa, uwaongoze njia yenye kheri na wao na uwahusu kwa mawaidha yako wale wanaotarajiwa kuwaidhika nayo. Wala usijisumbue kuwashauri wale ambao mawidha hayawaathiri isipokuwa kuwatia ujeuri na kuwafanya wayakimbie

Verse 10 — Surah Al-Ala 87:10

Atanufaika kwa mawaidha anayemcha Mola wke

Verse 11 — Surah Al-Ala 87:11

na atajiepusha na mawaidha aliye mbaya asiyemuogopa Mola wake

Verse 12 — Surah Al-Ala 87:12

atakayeingia kwenye Moto wa Jahanamu akiadhibika kwa ukali wake

Verse 13 — Surah Al-Ala 87:13

Kisha hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika wala ni mwenye kuishi akanufaika

Verse 14 — Surah Al-Ala 87:14

Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake na tabia mbovu

Verse 15 — Surah Al-Ala 87:15

na akamtaja Mwenyezi Mungu, akampwekesha, akamuomba, akafanya vitendo vya kumridhisha na akasimamisha Swala kwa nyakati zake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kufuata sheria Aliyoiweka

Verse 16 — Surah Al-Ala 87:16

Hakika yenu, nyinyi watu, mnafadhilisha pambo la maisha ya kilimwengu juu ya starehe za Akhera

Verse 17 — Surah Al-Ala 87:17

Na hakika ya mambo ni kuwa nyumba ya Akhera na starehe zake ni bora zaidi kuliko ulimwngu na ni yenye kusalia zaidi

Verse 18 — Surah Al-Ala 87:18

Haya mlioosimuliwa ndani ya Sura hii ni miongoni mwa yaliyotajwa kimaana katika Kurasa zilizotangulia kuteremshwa kabla ya Qur’ani

Verse 19 — Surah Al-Ala 87:19

Nazo ni Kurasa za Ibrāhīm na Mūsā, amani ziwashukie