Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 89 - Al-Fajr
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Fajr 89:1
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa alfajiri
Verse 2 — Surah Al-Fajr 89:2
na masiku kumi ya kwanza ya Mfungotatu na kwa kile kilichoyafanya yawe matukufu
Verse 3 — Surah Al-Fajr 89:3
kwa kila idadi igawanyikayo na isiyogawanyika
Verse 4 — Surah Al-Fajr 89:4
kwa usiku upitapo na giza lake
Verse 5 — Surah Al-Fajr 89:5
Kwani hakuna katika kiapo kiliyotajwa chenye kukinaisha kwa mwenye akili
Verse 6 — Surah Al-Fajr 89:6
Huoni, ewe Mtume, vipi Mola wako
Verse 7 — Surah Al-Fajr 89:7
Alivyoiangamiza kaumu ya Ād'. kabila la Irama lenye nguvu na majengo yaliyoinuliwa juu ya vipia
Verse 8 — Surah Al-Fajr 89:8
ambalo hakukuumbwa mfano wake katika miji, kwa ukubwa wa miili na wingi wa nguvu
Verse 9 — Surah Al-Fajr 89:9
Na vipi Alivyowafanya Thamūd, kaumu ya Ṣāliḥ, ambao waliweza kuchonga jabali na kufanya nyumba ndani yake
Verse 10 — Surah Al-Fajr 89:10
Na vipi Alivyomfanya Firauni, mfalme wa Misri, aliyekuwa na askari waliouhami ufalme wake na kuutilia nguvu
Verse 11 — Surah Al-Fajr 89:11
Hawa ndio waliokitumia nguvu na kudhulumu mijini
Verse 12 — Surah Al-Fajr 89:12
Wakaeneza humo, kwa dhuluma zao, uharibifu
Verse 13 — Surah Al-Fajr 89:13
Mwenyezi Mungu Akawamiminia adhabu kali
Verse 14 — Surah Al-Fajr 89:14
Hakika Mola wako,ewe Mtume, Anamwangalia mwenye kumuasi kwa kumpa muhula kidogo, kisha Humpatiliza kwa uwezo na ushindi
Verse 15 — Surah Al-Fajr 89:15
Huyu binadamu, Mola wake Anapompa mtihani wa neema, Anapomkunjulia riziki yake na kumpa maisha mazuri, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye ana cheo kwa Mola wake na huwa akisema :»Mola wangu Amenitukuza.»
Verse 16 — Surah Al-Fajr 89:16
Na Anapomuonja na Akambania riziki yake, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye amefanywa mnyonge na Mwenyezi Mungu na huwa akisema: «Mola wangu Amenifanya mnyonge.»
Verse 17 — Surah Al-Fajr 89:17
Hali ya mambo si kama anavyodhania binadamu huyu, kwani mtu hutukuzwa kwa kumtii Mwenyzi Mungu na hufanywa mnyonge kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamwakirimu mayatima na kuwatendea wema
Verse 18 — Surah Al-Fajr 89:18
Wala hamhimizani kulisha maskini
Verse 19 — Surah Al-Fajr 89:19
Na mnakula haki za watu, katika kurithi, kwa pupa
Verse 20 — Surah Al-Fajr 89:20
Na mnapenda mali kupita kiasi
Verse 21 — Surah Al-Fajr 89:21
Basi hali zenu zisiwe namna hiyo. Kumbukeni pindi ardhi itakapotikiswa na kuvunjwavunjwa
Verse 22 — Surah Al-Fajr 89:22
Na Akaja Mola wako kutoa uamuzi kwa waja Wake hali Malaika wamepiga safu
Verse 23 — Surah Al-Fajr 89:23
Na ukaletwa, Siku Hiyo kubwa, moto wa Jahanamu. Hiyo ndiyo Siku kafiri atakumbuka na kutubia. Kutamfalia nini sasa kukumbuka kwake na kutubia, na yeye katika ulimwengu alikuwa ameyapuuza hayo, na wakati wake umekwisha kupita
Verse 24 — Surah Al-Fajr 89:24
Atakuwa akisema: ‘Laiti mimi nilitanguliza ulimwenguni amali zenye kunifaa katika maisha yangu ya Akhera’
Verse 25 — Surah Al-Fajr 89:25
Katika Siku Hiyo ngumu yenye vituko, hakuna atakaye kuweza kuadhibu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa anayemuasi
Verse 26 — Surah Al-Fajr 89:26
Na hakuna atakaye kuweza kufunga kama kifungo Chake wala kufikia hadi yake
Verse 27 — Surah Al-Fajr 89:27
Ewe nafsi iliyotulia kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, kumwamini Yeye na kuamini starehe ya Pepo Aliyowaandalia waumini
Verse 28 — Surah Al-Fajr 89:28
Rudi kwa Mola wako hali ya kuridhika na takrima ya Mwenyezi Mungu kwako na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ameridhika na wewe
Verse 29 — Surah Al-Fajr 89:29
Ingia miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu walio wema
Verse 30 — Surah Al-Fajr 89:30
na ingia kwenye Pepo yangu