Back to Languages

Swahili - Chapter 90 - Al-Balad

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Balad 90:1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mji huu mtakatifu wa Makkah

Verse 2 — Surah Al-Balad 90:2

Na wewe, ewe Nabii, ni mkazi wa mji huu mtakatifu

Verse 3 — Surah Al-Balad 90:3

Na Anaapa kwa mzazi wa wanaadamu, ambaye ni Ādam, amani imshukie, na kilichozalikana na yeye

Verse 4 — Surah Al-Balad 90:4

Hakika Tumemuumba binadamu katika usumbufu na shida za kilimwengu

Verse 5 — Surah Al-Balad 90:5

Kwani anadhani kwa mali aliyoyakusanya kuwa Mwenyezi Mungu Hatakuwa na uwezo juu yake

Verse 6 — Surah Al-Balad 90:6

Huwa akisema kwa kujigamba: «Nimetumia mali mengi.»

Verse 7 — Surah Al-Balad 90:7

Kwani anadhani, kwa kitendo chake hiko, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, Hamuoni wala hatamhesabu juu ya kubwa na dogo

Verse 8 — Surah Al-Balad 90:8

Kwani hatukumpa macho mawili ya kuonea

Verse 9 — Surah Al-Balad 90:9

ulimi na midomo miwili ya kusemea

Verse 10 — Surah Al-Balad 90:10

na kumfafanulia njia mbili: ya kheri na ya shari

Verse 11 — Surah Al-Balad 90:11

Basi ajiepushe na janga la Akhera kwa kutoa mali yake ili aokoke

Verse 12 — Surah Al-Balad 90:12

Ni kitu gani kilichojulisha ni lipi hilo janga la Akhera na ni mambo gani yenye kusaidia kujiepusha nalo

Verse 13 — Surah Al-Balad 90:13

Ni kuacha huru shingo iliyoamini kuikomboa na utumwa

Verse 14 — Surah Al-Balad 90:14

Au kulisha, wakati wa shida ya njaa

Verse 15 — Surah Al-Balad 90:15

yatima mwenye ujamaa, ili ipatikane fadhila ya sadaka na ya kuunga kizazi

Verse 16 — Surah Al-Balad 90:16

au masikini asiyekuwa na kitu

Verse 17 — Surah Al-Balad 90:17

Kisha akawa, baada ya kufanya amali njema zilizotajwa, ni miongoni mwa waliotakasa Imani yao kwa Mwenyezi Mungu, wakausiana kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi na wakausiana kuwahurumia viumbe

Verse 18 — Surah Al-Balad 90:18

Wenye kufanya hayo ndiwo watu wa kulia ambao watapelekwa Siku ya Kiyama upande wa kulia kuelekea Peponi

Verse 19 — Surah Al-Balad 90:19

Na wale waliokanusha Qur’ani ndio ambao watapelekwa, Siku ya Kiyama, upande wa kushoto kuelekea Motoni

Verse 20 — Surah Al-Balad 90:20

Malipo yao ni Moto wa Jahanamu wenye kuwafinika na kuwaziba