Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 91 - Ash-Shams
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah Ash-Shams 91:1
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa jua na mchana wake na mwangaza wake wa asubuhi
Verse 2 — Surah Ash-Shams 91:2
Na kwa mwezi unapolifuata wakati wa kucha na kutwa
Verse 3 — Surah Ash-Shams 91:3
Na kwa mchana unapoliondoa giza na kulifunua
Verse 4 — Surah Ash-Shams 91:4
Na kwa usiku unapoifinika ardhi ikawa giza
Verse 5 — Surah Ash-Shams 91:5
Na kwa mbingu na kujengeka kwake kiimara
Verse 6 — Surah Ash-Shams 91:6
Na kwa ardhi na kutandikika kwake
Verse 7 — Surah Ash-Shams 91:7
Na kwa kila nafsi na namna Mwenyezi Mungu alivyoikamilisha umbo lake ili itekeleze kazi iliyoumbiwa nayo
Verse 8 — Surah Ash-Shams 91:8
Akaibainishia njia ya shari na njia ya kheri
Verse 9 — Surah Ash-Shams 91:9
Amefaulu mwenye kuisafisha na kuikuza kwa kheri
Verse 10 — Surah Ash-Shams 91:10
Na ameingia kwenye hasara mwenye kuitia nafsi yake kwenye maasia
Verse 11 — Surah Ash-Shams 91:11
Kabila la Thamūd lilimkanusha Nabii wake kwa kuvama kwenye uasi
Verse 12 — Surah Ash-Shams 91:12
Pindi walipotoka wabaya zaidi wa kabila hilo kumchinja Ngamia. Mtume wa Mwenyezi Mungu’ Ṣāliḥ, amani imshukie
Verse 13 — Surah Ash-Shams 91:13
akawaambia: «Tahadharini kumgusa kwa ubaya ngamia ambaye ni miujiza ilioletwa na Mwenyezi Mungu kwenu inayoonyesha ukweli wa Nabii wenu, na msizuie kinywaji chake. Yeye ana siku yake ya kunywa na nyinyi mna siku yenu maalumu ya kunywa.» Hilo likawa zito kwao
Verse 14 — Surah Ash-Shams 91:14
Wakamkanusha na kulipuza onyo lake wakamchinja.Mola wao Akawafinika kwa adhabu, akaisawazisha juu yao na hakuna aliyeweza kuponyoka
Verse 15 — Surah Ash-Shams 91:15
Wala Haogopi, Mwenye uwezo uliotukuka, athari ya adhabu kali Aliywateremshia