Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 92 - Al-Layl
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Layl 92:1
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake
Verse 2 — Surah Al-Layl 92:2
Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku
Verse 3 — Surah Al-Layl 92:3
Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike
Verse 4 — Surah Al-Layl 92:4
Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera
Verse 5 — Surah Al-Layl 92:5
Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa
Verse 6 — Surah Al-Layl 92:6
akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo
Verse 7 — Surah Al-Layl 92:7
Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake
Verse 8 — Surah Al-Layl 92:8
Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake
Verse 9 — Surah Al-Layl 92:9
akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo
Verse 10 — Surah Al-Layl 92:10
Tutamnyoshea njia za mateso
Verse 11 — Surah Al-Layl 92:11
Wala hayatamfaa yeye mali yake aliyoyafanyia ubakhili atakapotumbukia Motoni
Verse 12 — Surah Al-Layl 92:12
Ni juu Yetu, kwa fadhila Zetu na busara Yetu, kueleza njia ya uongofu yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na ya upotevu
Verse 13 — Surah Al-Layl 92:13
Na Sisi Tuna mamlaka ya maisha ya Akhera na maisha ya ulimwenguni
Verse 14 — Surah Al-Layl 92:14
Ndipo nikawaonya , enyi watu, na kuwatisha moto wenye kuwaka, nao ni moto wa Jahanamu
Verse 15 — Surah Al-Layl 92:15
Hataingia Moto huo isipokuwa aliyekuwa mbaya sana. Mwenye kumkanusha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
Verse 16 — Surah Al-Layl 92:16
na akakataa kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake
Verse 17 — Surah Al-Layl 92:17
Na ataepushwa nao mchaji Mwenyezi Mungu sana
Verse 18 — Surah Al-Layl 92:18
Ambaye hutoa mali yake kwa kutaka nyongeza za kheri
Verse 19 — Surah Al-Layl 92:19
kutoa Kwake si kwa kulipa zema alizofanyiwa na mtu
Verse 20 — Surah Al-Layl 92:20
Lakini anatoa kwa kutaka uso wa Mola wake na radhi zake. Basi Mwenyezi Mungu atampa
Verse 21 — Surah Al-Layl 92:21
huko Peponi, malipo ya kumridhisha