Back to Languages

Swahili - Chapter 95 - At-Tin

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah At-Tin 95:1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa tini na zaituni, nayo ni miongoni mwa matunda yanayojulikana

Verse 2 — Surah At-Tin 95:2

Na Anaapa kwa jabali la Ṭūr Sīnā’ ambalo Mwenyezi Mungu Alisema na Mūsā juu yake

Verse 3 — Surah At-Tin 95:3

Na Anaapa kwa Mji huu wa amani, usiokuwa na mambo ya kutisha. Nao ni mji wa Makkah, chimbuko la Uislamu

Verse 4 — Surah At-Tin 95:4

Hakika Tumemuumba binadamu katika sura nzuri

Verse 5 — Surah At-Tin 95:5

Kisha Tutampeleka Motoni akiwa hakumtii Mweyezi Mungu na hakuwafuata Mitume

Verse 6 — Surah At-Tin 95:6

Isipokuwa wale walioamini na wakafanya amali njema; wao watakuwa na malipo makubwa yasiyokatika wala kupungua

Verse 7 — Surah At-Tin 95:7

Ni lipi linalokupelekea wewe, ewe binadamu, kukanusha kufufuliwa na kulipwa, hali ya kuwa kuna dalili wazi kwamba Mwenyezi Mungu Ana uweza wa kufanya hayo

Verse 8 — Surah At-Tin 95:8

Je, Hakuwa Mwenyezi Mungu , Ambaye Ameiweka Siku hii kutoa uamuzi baina ya watu, ni muadilifu zaidi ya wanaosifika kuwa ni waadilifu katika kila Alichokiumba? Kwani? Alikuwa. Basi wataachwa viumbe rebe: hawaamrishwi wala hawakatazwi wala hawalipwi kwa mema wala hawateswi kwa mabaya? Hilo si sahihi wala haliwi