Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 97 - Al-Qadr
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Qadr 97:1
Sisi Tumeiteremsha Qur’ani katika usiku wa cheo na utukufu , nao ni moja wa masiku ya mwezi wa Ramdhani
Verse 2 — Surah Al-Qadr 97:2
Na nilipi liliokujulisha, ewe Mtume, ni upi usiku wa cheo na utukufu
Verse 3 — Surah Al-Qadr 97:3
Usiku wa cheo na utukufu ni bora fadhila zake kuliko fadhila za miezi elfu moja isiyokuwa usiku huo
Verse 4 — Surah Al-Qadr 97:4
Usiku huo hushuka Malaika na Jibrili, amani iwashukie, kwa ruhusa ya Mola wao kwa kila jambo Alilolikadiria liwe mwaka huo
Verse 5 — Surah Al-Qadr 97:5
Usiku huo wote ni amani, hakuna shari, mpaka kutokea alfajiri