Back to Languages

Swahili - Chapter 46 - Al-Ahqaf

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 20 — Surah Al-Ahqaf 46:20

Na siku watakapo letwa walio kufuru kwenye Moto wataambiwa: Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika uhai wa duniani, na mkastareheshwa navyo. Basi leo ndio mnalipwa adhabu ya fedheha kwa mlivyo kuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa sababu mlikuwa mkifanya upotovu