Back to Languages

Swahili - Chapter 48 - Al-Fath

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 15 — Surah Al-Fath 48:15

Walio baki nyuma watasema: Mtapo kwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni! Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu. Sema: Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema kama hivi zamani. Hapo watasema: Bali nyinyi mnatuhusudu. Siyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo