Back to Languages

Swahili - Chapter 58 - Al-Mujadila

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Mujadila 58:1

MWENYEZI MUNGU amekwisha sikia usemi wa mwanamke anaye jadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona