Back to Languages

Swahili - Chapter 9 - At-Tawbah

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 71 — Surah At-Tawbah 9:71

Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima