Back to Languages

Swahili - Chapter 100 - Al-Adiyat

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Adiyat 100:1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda shoti katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina

Verse 2 — Surah Al-Adiyat 100:2

Na wenye kutoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi

Verse 3 — Surah Al-Adiyat 100:3

Wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi

Verse 4 — Surah Al-Adiyat 100:4

Wakarusha vumbi kwa mbio zao

Verse 5 — Surah Al-Adiyat 100:5

Wakautia kati, kwa kuuzunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui

Verse 6 — Surah Al-Adiyat 100:6

Hakika binadamu ni mkanushaji sana neema za Mola wake

Verse 7 — Surah Al-Adiyat 100:7

Na yeye anakubali ukanushaji wake

Verse 8 — Surah Al-Adiyat 100:8

Na yeye ana pupa sana la mali

Verse 9 — Surah Al-Adiyat 100:9

Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa

Verse 10 — Surah Al-Adiyat 100:10

Na (kwani yeye hajui) yakatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema au maovu

Verse 11 — Surah Al-Adiyat 100:11

Hakika Mola wao kwao na kwa amali zao, Siku Hiyo, ni Mtambuzi; hakuna chenye kufichamana Kwake