Back to Languages

Swahili - Chapter 99 - Az-Zalzalah

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Az-Zalzalah 99:1

Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu

Verse 2 — Surah Az-Zalzalah 99:2

Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandi

Verse 3 — Surah Az-Zalzalah 99:3

Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?»

Verse 4 — Surah Az-Zalzalah 99:4

Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya

Verse 5 — Surah Az-Zalzalah 99:5

kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa

Verse 6 — Surah Az-Zalzalah 99:6

Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo

Verse 7 — Surah Az-Zalzalah 99:7

Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera

Verse 8 — Surah Az-Zalzalah 99:8

Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera