Back to Languages

Swahili - Chapter 103 - Al-Asr

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Asr 103:1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa zama

Verse 2 — Surah Al-Asr 103:2

kwamba wanadamu wako kwenye maangamivu na upungufu. Haifai kwa mja kuapa isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, kwani kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina

Verse 3 — Surah Al-Asr 103:3

Isipokuwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakafanya amali njema, wakausiana wao kwa wao kushikamana na haki, kufanya matendo ya kumtii Mwenyezi Mungu na kusubiri juu yake