Back to Languages

Swahili - Chapter 104 - Al-Humazah

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Humazah 104:1

Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana

Verse 2 — Surah Al-Humazah 104:2

Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuyahesabu

Verse 3 — Surah Al-Humazah 104:3

Akidhani kuwa mali yake ambayo ameyakusanya yatampa dhamana ya kuishi milele duniani na kuhepa kuhesabiwa

Verse 4 — Surah Al-Humazah 104:4

Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa

Verse 5 — Surah Al-Humazah 104:5

Lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni upi huo Moto unaovunjavunja

Verse 6 — Surah Al-Humazah 104:6

Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa

Verse 7 — Surah Al-Humazah 104:7

Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo

Verse 8 — Surah Al-Humazah 104:8

Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo

Verse 9 — Surah Al-Humazah 104:9

na pingu ndefu ili wasitoke