Back to Languages

Swahili - Chapter 109 - Al-Kafirun

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Kafirun 109:1

Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu

Verse 2 — Surah Al-Kafirun 109:2

«Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo

Verse 3 — Surah Al-Kafirun 109:3

«Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwa

Verse 4 — Surah Al-Kafirun 109:4

«Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo

Verse 5 — Surah Al-Kafirun 109:5

«Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Mwenyezi Mungu Alijua kuwa hawataamini kabisa

Verse 6 — Surah Al-Kafirun 109:6

«Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.»