Back to Languages

Swahili - Chapter 111 - Al-Masad

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Masad 111:1

Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutu

Verse 2 — Surah Al-Masad 111:2

Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukia

Verse 3 — Surah Al-Masad 111:3

Ataingia kwenye Moto wenye kuroroma

Verse 4 — Surah Al-Masad 111:4

yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi

Verse 5 — Surah Al-Masad 111:5

Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini