Back to Languages

Swahili - Chapter 69 - Al-Haqqah

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Haqqah 69:1

Kiyama chenye kutukia kikweli ambacho ndani yake inahakikika ahadi ya Mwenyezi Mungu na onyo Lake

Verse 2 — Surah Al-Haqqah 69:2

Kiyama chenye kutukia kikweli ni zipi sifa zake na hali zake

Verse 3 — Surah Al-Haqqah 69:3

Na kitu gani kilichokujulisha wewe, ewe Mtume, na kukueleza uhakika wa Kiyama na kikakupa wewe picha ya janga lake na shida zake

Verse 4 — Surah Al-Haqqah 69:4

Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, na ‘Ād, nao ni watu wa Hūd, walikikanusha Kiyama ambacho kinagonga nyoyo kwa vituko janga lake

Verse 5 — Surah Al-Haqqah 69:5

Ama hao Thamūd waliangamizwa kwa ukelele mkubwa uliopita kiasi ukali wake

Verse 6 — Surah Al-Haqqah 69:6

na ama‘Ād waliangamizwa kwa upepo baridi unaovuma kwa nguvu

Verse 7 — Surah Al-Haqqah 69:7

Mwenyezi Mungu Aliwasaliti nao masiku saba na michana minane yenye kufuatana, isiyokatika wala kusimama. Utawaona watu katika masiku hayo na michana wamekufa, kama kwamba wao ni vigogo mitende iliyo mibovu iliyolika ndani

Verse 8 — Surah Al-Haqqah 69:8

Basi je utamuona mtu yoyote miongoni mwao mwenye kusalia bila kuangamia

Verse 9 — Surah Al-Haqqah 69:9

Na akaja mpita kiasi katika uasi Fir’awn na ummah waliomtangulia waliokanusha Mitume wao, na watu wakazi wa vijiji vya watu wa Lūṭ ambao majumba yao yaliwapindukia kwa sababu ya kitendo kibaya walichokifanya, cha ukafiri, ushirikina na mambo machafu

Verse 10 — Surah Al-Haqqah 69:10

Kila ummah kati yao walimuasi mjumbe wa Mola wao ambaye alitumwa kwao, basi Mwenyezi Mungu Akawashika mshiko mkali mno

Verse 11 — Surah Al-Haqqah 69:11

Sisi, maji yalipopita kipimo chake, mpaka yakawa juu na kuangatika juu ya kila kitu, tuliwabeba watu wa asili zenu pamoja na Nūḥ ndani ya jahazi ambayo ilikuwa ndio sababu ya kuokoka Waumini na kuzamishwa makafiri

Verse 12 — Surah Al-Haqqah 69:12

hili likiwa ni mazingatio na mawaidha, na lipate kulihifadhi tukio hilo kila shikio ambalo kazi yake ni kuhifadhi, na lielewe kile ambacho limekisikia

Verse 13 — Surah Al-Haqqah 69:13

Pindi Malaika atakapopuliza kwenye barugumu mpulizo mmoja, nao ni mpulizo wa kwanza ambao hapo patapatikana maangamivu ya ulimwengu

Verse 14 — Surah Al-Haqqah 69:14

Na pindi ardhi na milima itakapoinuliwa kutoka mahali ilipo ikavunjwavunjwa na kugongwagongwa mara moja

Verse 15 — Surah Al-Haqqah 69:15

Wakati huo Kiyama kitasimama

Verse 16 — Surah Al-Haqqah 69:16

Na mbingu zitafanya ufa na ziwe dhaifu na kulegea Siku hiyo, hazitakuwa na mshikamano wala ugumu

Verse 17 — Surah Al-Haqqah 69:17

Na Malaika watakuwa kwenye pambizo na pande zake, na wataibeba «Arshi ya Mola wako juu yao Siku ya Kiyama Malaika wanane miongoni mwa Malaika wakubwa

Verse 18 — Surah Al-Haqqah 69:18

Katika Siku hiyo, mtaorodheshwa kwa Mwenyezi Mungu, enyi wat, ili mhesabiwe na mlipwe, hakuna chochote kitakachofichamana kwa Mwenyewzi Mungu miongoni mwa siri zenu

Verse 19 — Surah Al-Haqqah 69:19

Ama yule Atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwa katika hali ya ubashasha na furaha, ‘Chukueni kitabu changu mkisome

Verse 20 — Surah Al-Haqqah 69:20

Mimi nilikuwa na yakini duniani kuwa nitapata malipo yangu Siku ya Kiyama, nikajiandalia nayo kwa matayarisho ya Imani na matendo mema.»

Verse 21 — Surah Al-Haqqah 69:21

Basi yeye atakuwa kwenye maisha ya furaha ya kumridhisha

Verse 22 — Surah Al-Haqqah 69:22

kwenye Pepo ya juu kimahali na daraja

Verse 23 — Surah Al-Haqqah 69:23

matunda yake yako karibu, anayachuma anayesimama, anayeketi na anayelala

Verse 24 — Surah Al-Haqqah 69:24

Wataambiwa, «Kuleni na mnyweni kila aina ya vyakula na vinywaji, mkiwa mbali na kila kero, mkiwa mmesalimika na kila mnalolichukia, kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza siku za ulimwenguni.»

Verse 25 — Surah Al-Haqqah 69:25

Na ama yule atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kushoto

Verse 26 — Surah Al-Haqqah 69:26

atasema akiwa katika hali ya kujuta na kupata hasara

Verse 27 — Surah Al-Haqqah 69:27

«Natamani lau mimi sikupewa kitabu changu na sikujua malipo yangu! Natamani lau kile kifo nilichokufa duniani kilikuwa ndicho chenye kukata kabisa mambo yangu na nisifufuliwe baada yake

Verse 28 — Surah Al-Haqqah 69:28

Mali yangu niliyoyakusanya hayakuninufaisha duniani

Verse 29 — Surah Al-Haqqah 69:29

Hoja zangu zote zimenionokea, na sina hoja tena ya kuitumia kama hoja.»

Verse 30 — Surah Al-Haqqah 69:30

Hapo waambiwe walinzi wa Moto wa Jahanamu, «Mchukueni mhalifu huyu mfanya dhambi, ikusanyeni mikono yake shingoni mwake muitie pingu

Verse 31 — Surah Al-Haqqah 69:31

kisha mtieni kwenye Moto unaowaka sana, apate kulihisi joto lake

Verse 32 — Surah Al-Haqqah 69:32

Kisha mfungeni mnyororo wa chuma ambao urefu wake ni dhiraa sabini mumkokote nao na mumtie humo

Verse 33 — Surah Al-Haqqah 69:33

Kwani yeye hakuwa akiamini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa Haki, Peke Yake, Asiye na mshirika

Verse 34 — Surah Al-Haqqah 69:34

Wala hakuwa akitenda matendo yanayoambatana na uongofu Wake, wala hakuwa akiwahimiza watu duniani kuwalisha wenye uhitaji miongoni mwa masikini na wengineo

Verse 35 — Surah Al-Haqqah 69:35

basi kafiri huyu Siku ya Kiyama hatakuwa na jamaa wa karibu wa kumuepushia adhabu

Verse 36 — Surah Al-Haqqah 69:36

wala hatakuwa na chakula isipokuwa kile kinachotokana na usaa wa watu wa motoni

Verse 37 — Surah Al-Haqqah 69:37

hakuna mwenye kukila isipokuwa wale wenye dhambi, wanaoshikilia kumkanusha Mwenyezi mungu

Verse 38 — Surah Al-Haqqah 69:38

Naapa kwa mnavyoviona miongoni mwa vitu vinavyooonekana

Verse 39 — Surah Al-Haqqah 69:39

na vile msivyoviona miongoni mwa vile vilivyoghibu kwenu., hakika Qur’ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu

Verse 40 — Surah Al-Haqqah 69:40

Inasomwa na mjumbe mkubwa wa cheo na utukufu

Verse 41 — Surah Al-Haqqah 69:41

Na si maneno ya mshairi kama mnavyodai, ni uchache mno mnavyoamini

Verse 42 — Surah Al-Haqqah 69:42

Wala si tungo kama zile tungo za makuhani, ni kuchache mno kule kukumbuka kwenu na kutia akilini kuwa kuna tafauti baina ya mawili hayo

Verse 43 — Surah Al-Haqqah 69:43

Lakini hiyo Qur’ani ni maneno ya Mola wa viumbe wote Aliyoyateremshia Mtume Wake Muhaammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

Verse 44 — Surah Al-Haqqah 69:44

Na lau Muhammad angalitusingizia maneno tusiyoyanena

Verse 45 — Surah Al-Haqqah 69:45

tungalimtesa na tungalimkamata kwa nguvu na uweza, kwani nguvu ya kila kitu iko kwenye upande wake wa kulia

Verse 46 — Surah Al-Haqqah 69:46

kisha tungalimkata mshipa wa moyo wake

Verse 47 — Surah Al-Haqqah 69:47

hataweza yoyote kuyazuia mateso yetu yasimpate

Verse 48 — Surah Al-Haqqah 69:48

Na hii Qur’ani ni mawaidha kwa wachamungu wanaofuata amri za Mwenyezi Mungu na kuyaepuka makatazo yake

Verse 49 — Surah Al-Haqqah 69:49

Na sisi kwa hakika tunajua kwamba miongoni mwenu kuna wanaoikanusha hii Qur’ani pamoja na kuwa dalili zake ziko wazi

Verse 50 — Surah Al-Haqqah 69:50

Na kwa hakika kuikanusha Qur’ani ni majuto makubwa kwa wenye kuikanusha pindi watakapoiona adhabu yao na kuona starehe za wenye kuiamini

Verse 51 — Surah Al-Haqqah 69:51

Na kwa hakika hii Qur’ani ni haki iliyothibiti na yakini isiyo na shaka

Verse 52 — Surah Al-Haqqah 69:52

Basi Mwepushie Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kila sifa isiyonasibiana na haiba Yake, na umtaje kwa jina Lake tukufu