Back to Languages

Swahili - Chapter 70 - Al-Maarij

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Maarij 70:1

Ameapiza mwenye kuapiza miongoni mwa washirikina, kujiapiza mwenyewe na kuwaapiza watu wake kuteremkiwa na adhabu

Verse 2 — Surah Al-Maarij 70:2

nayo ni yenye kuwashukia bila shaka Siku ya Kiyama

Verse 3 — Surah Al-Maarij 70:3

Hakuna mzuiaji yoyote wa kuizuia isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenye utukufu na haiba

Verse 4 — Surah Al-Maarij 70:4

Malaika na Jibrili wanapanda kuenda Kwake, Aliyetukuka, kwa siku moja ambayo kadiri yake ni myaka elfu hamsini katika myaka ya duniani, nayo kwa aliyeamini ni kama muda wa Swala moja ya faradhi

Verse 5 — Surah Al-Maarij 70:5

Basi vumilia, ewe Mtume, kule kufanya kwao shere na kutaka kwao wafikiwe na adhabu kwa haraka, uvumilivu usiokuwa na babaiko wala kumshtakia asiyekuwa Mwenyezi Mungu

Verse 6 — Surah Al-Maarij 70:6

Kwa kweli makafiri wanaiona adhabu kuwa iko mbali na wanaona kuwa si yenye kutukia

Verse 7 — Surah Al-Maarij 70:7

Na sisi tunaiona ni yenye kutukia kwa kipindi cha karibu bila shaka

Verse 8 — Surah Al-Maarij 70:8

Siku ambayo mbingu itayayuka iwe ni kama rojo la mafuta

Verse 9 — Surah Al-Maarij 70:9

na majabali yawe ni kama sufi iliyochanganywa na iliyoshanuliwa na kupeperushwa na upepo

Verse 10 — Surah Al-Maarij 70:10

Wala mtu hatamuuliza jamaa yake wa karibu kuhusu jambo lake, kwani kila mmoja ameshughulishwa na nafsi yake

Verse 11 — Surah Al-Maarij 70:11

Watawaona na watawajua, na hakuna yoyote atakayeweza kumnufaisha yoyote. Kafiri atatamani lau ajikomboa nafsi yake na adhabu ya Siku ya Kiyama kwa watoto wake

Verse 12 — Surah Al-Maarij 70:12

Verse 13 — Surah Al-Maarij 70:13

jamaa zake wanaomuhami na ambao anajinasibisha nao kwa ujamaa

Verse 14 — Surah Al-Maarij 70:14

na kwa wote walio kwenye ardhi miongoni mwa binadamu na wengineo ili aokoke na adhabu ya Mwenyezi Mungu

Verse 15 — Surah Al-Maarij 70:15

Mambo siyo kama vile unavyotamani yawe, ewe kafiri, ya kujikomboa

Verse 16 — Surah Al-Maarij 70:16

Huo ni moto wa Jahanamu, moto wake unawaka na kuroroma, joto lake linatoa kwa nguvu ngozi ya kichwa na sehemu nyingine za mwili

Verse 17 — Surah Al-Maarij 70:17

unamwita aliyeipa mgongo haki duniani na akaacha kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake

Verse 18 — Surah Al-Maarij 70:18

na akakusanya mali na kuyaweka kwenye mahazina yake na asitekeleze amri ya Mwenyezi Mungu kwenye mali hayo

Verse 19 — Surah Al-Maarij 70:19

Hakika binadamu ameumbwa akiwa na tabia ya babaiko na pupa

Verse 20 — Surah Al-Maarij 70:20

Yakimpata makero na shida, anababaika sana na kufa moyo

Verse 21 — Surah Al-Maarij 70:21

Na yakimpata mambo mazuri na ukunjufu wa maisha, huwa ni mwingi wa kuzuia na

Verse 22 — Surah Al-Maarij 70:22

Isipokuwa wenye kusimamisha Swala

Verse 23 — Surah Al-Maarij 70:23

wanaochunga kuitekeleza katika nyakati zake zote, hakuna shughuli yoyote inayowashughulisha nayo

Verse 24 — Surah Al-Maarij 70:24

Na wale ambao katika mali yao kuna fungu maalumu alililowafaradhia Mwenyezi Mungu, nalo ni Zaka

Verse 25 — Surah Al-Maarij 70:25

wanaozitoa kwa anayeomba msaada na kwa na kwa asiyeomba

Verse 26 — Surah Al-Maarij 70:26

Na wale ambao wanaiamini Siku ya kuhesabiwa na kulipwa wakajiandaa nayo kwa matendo mema

Verse 27 — Surah Al-Maarij 70:27

Na wale ambao wao wanaiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu

Verse 28 — Surah Al-Maarij 70:28

kwani adhabu ya Mola wao haipaswi kwa yoyote kujiaminisha nayo

Verse 29 — Surah Al-Maarij 70:29

Na wale ambao wao ni wenye kutunza tupu zao na kila alichokiharamishia Mwenyezi Mungu

Verse 30 — Surah Al-Maarij 70:30

isipokuwa wake zao na vijakazi vyao, hakika wao kwa hao hawapatilizwi

Verse 31 — Surah Al-Maarij 70:31

Basi mwenye kutaka kumaliza matamanio yake ya kimwili kwa wasiokuwa wake zake au vijakazi vyake, basi hao ndio wenye kukiuka mipaka ya halali kuingia kwenye haramu

Verse 32 — Surah Al-Maarij 70:32

Na wale ambao wanazitunza amana za Mwenyezi Mungu na amana za waja, na wanatunza ahadi zao pamoja na Mwenyezi Munmgu, Aliyetukuka, na pamoja na waja

Verse 33 — Surah Al-Maarij 70:33

Na wale ambao wanatekeleza ushahidi wao kwa ukweli bila kubadilisha au kuficha

Verse 34 — Surah Al-Maarij 70:34

Na wale ambao wanatunza utekelezaji Swala wala hawaharibu chochote cha wajibu katika hiyo Swala

Verse 35 — Surah Al-Maarij 70:35

Hao waliosifika kwa sifa hizo njema, ni wenye kutulia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe, ni wenye kukirimiwa humo kwa kila aina ya takrima

Verse 36 — Surah Al-Maarij 70:36

Ni msukumo gani unaowasukuma makafiri watembee kwa haraka kuelekea upande wako, ewe Mtume, na huku wamenyosha shingo zao kwako, wamekukabili kwa macho yao

Verse 37 — Surah Al-Maarij 70:37

wanajikusanya kuliani kwako na kushotoni kwako, wakiwa wamekaa kwa kupiga maduara na wamejigawa vikundi mbalimbali, wanazungumza na kuona ajabu

Verse 38 — Surah Al-Maarij 70:38

Je ana tamaa kila mmoja miongoni mwa makafiri kuwa Mwenyezi Mungui Atamuingiza kwenye Pepo ya starehe ya daima? Mambo siyo kama vile wanavyotazamia. Wao hawataiingia hiyo Pepo kabisa

Verse 39 — Surah Al-Maarij 70:39

Hakika sisi tumewaumba kwa kile wanachokijua cha maji matwevu kama wengineo, na vilevile hawakuamini. Basi vipi watapata heshima ya kuingia Pepo ya sterehe

Verse 40 — Surah Al-Maarij 70:40

Sivyo hivyo. Najiapia Mimi Mwenyewe niliye Mola wa pande za kuchomoza na kutua jua, mwezi na sayari nyinginezo, kwa yanayopatikana humo miongoni mwa dalili waziwazi za kujulisha kufufuliwa

Verse 41 — Surah Al-Maarij 70:41

kuwa Sisi tunaweza kuwaleta watu badala yao walio bora zaidi kuliko wao na watiifu zaidi wa Mwenyezi Mungu. Na hakuna yoyote atakayetushinda na kutuponyoka na kutuelemea iwapo tunataka kumrudisha uhai baada ya kufa

Verse 42 — Surah Al-Maarij 70:42

Basi waache wavame kwenye ubatilifu wao na wacheze kwenye ulimwengu wao mpaka wakutane na Siku ya Kiyama ambayo wanaahidiwa kuwa wataadhibiwa

Verse 43 — Surah Al-Maarij 70:43

Siku watakapotoka makaburini wakienda kwa haraka, kama wlivyokuwa duniani wakienda mbio na haraka kwa waungu wao wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu

Verse 44 — Surah Al-Maarij 70:44

hali ya kuwa macho yao ni madhalilifu yanatazama chini, wamefinikwa na unyonge na utwevu. Hiyo ndiyo Siku waliyoahidiwa duniani na walikuwa wakiifanyia shere na kuikanusha