Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 79 - An-Naziat
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah An-Naziat 79:1
Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Malaika ambao huzing’oa roho za makafiri mng’oo mkali
Verse 2 — Surah An-Naziat 79:2
Na kwa Malaika ambao huzitukua roho za Waumini kwa uchangamfu na upole
Verse 3 — Surah An-Naziat 79:3
Na kwa Malaika wanaoogelea katika kushuka kwao kutoka mbinguni na kupaa kwao kwenda mbinguni
Verse 4 — Surah An-Naziat 79:4
Na kwa Mlaika ambao wanakimbilia kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu
Verse 5 — Surah An-Naziat 79:5
Na kwa Malaika wanaopitisha amri za Mola wao katika mambo ya ulimwengu waliowakilishwa kuyafanya na kuyasimamia, - Wala haifai kwa kiumbe kukiapia chochote kile, bali yapasa kiapo chake kiwe ni kwa jina la Mola wake Muumba au sifa Zake. Na lau ataapa kwa asiye Muumba wake, basi huyo amekuwa mshirikina - Watafufuliwa viumbe bila shaka na watahesabiwa
Verse 6 — Surah An-Naziat 79:6
Siku ambayo ardhi itatetemeka kwa mvuvuo wa kwanza
Verse 7 — Surah An-Naziat 79:7
mvuvio wa kufisha, ukifuatiwa na mvuvio mwingine wa kuhuisha
Verse 8 — Surah An-Naziat 79:8
Nyoyo za makafiri, Siku hiyo, zitakuwa na papatiko kwa kicho kikubwa
Verse 9 — Surah An-Naziat 79:9
Macho ya makafiri hao yatakuwa madhalilifu kwa kitisho watakachokiona
Verse 10 — Surah An-Naziat 79:10
Wanasema hawa wakanushao kufufuliwa
Verse 11 — Surah An-Naziat 79:11
«Je, tutarudishwa baada ya kufa kwetu kwenye yale tuliyokuwa nayo katika ardhi? Je, tutarudishwa na hali tushakuwa mifupa iliochakaa?»
Verse 12 — Surah An-Naziat 79:12
Wakasema: «Kurejea kwetu huko kutakuwa kutupu kusikokuwa kweli.’
Verse 13 — Surah An-Naziat 79:13
Hakika tukio hilo litakuwa kwa mvivio mmoja tu
Verse 14 — Surah An-Naziat 79:14
Wakitahamaki wao wako hai juu ya ardhi baada ya kuwa walikuwa ndani yake
Verse 15 — Surah An-Naziat 79:15
Je imekujilia, ewe Mtume, habari ya Mūsā
Verse 16 — Surah An-Naziat 79:16
Pindi Mola wake Alipomwita katika bonde lililotakaswa na kubarikiwa, la Ṭuwā. Akamwambia
Verse 17 — Surah An-Naziat 79:17
«Enda kwa Firauni. Hakika yeye amekiuka mno katika kuasi
Verse 18 — Surah An-Naziat 79:18
Ukamwambie, ‘Je, unapendelea kuitakasa nafsi yako na upungufu na kuipamba na imani
Verse 19 — Surah An-Naziat 79:19
Na nikuelekeze njia ya kumtii Mola wako, upate kumcha na kumuogopa?’»
Verse 20 — Surah An-Naziat 79:20
Mūsā alimuonyesha Firauni alama kubwa: fimbo na mkono
Verse 21 — Surah An-Naziat 79:21
Hapo Firauni alimkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu , naye ni Mtume Mūsā, amani imshukie, na alimuasi Mola wake Aliyetukuka
Verse 22 — Surah An-Naziat 79:22
Kisha alikengeuka hali ya kuipa mgongo Imani na kufanya bidii katika kumpinga Mūsā
Verse 23 — Surah An-Naziat 79:23
Hapo aliwakusanya raia wa utawala wake na akawaita kwa
Verse 24 — Surah An-Naziat 79:24
kuwaambia,»Mimi ndiye mola wenu ambaye hakuna mola mwengine aliye juu yake.»
Verse 25 — Surah An-Naziat 79:25
Hapo Mwenyezi Mungu Alimtesa kwa adhabu ya duniani na ya Akhera
Verse 26 — Surah An-Naziat 79:26
Na Akaifanya adhabu hiyo iwe ni mazingatio na ni onyo kwa watu mfano wake kati ya wale waasi. Hakika Firauni na kile kilichompata cha adhabu ni mawaidha kwa mwenye kuwaidhika na kutishika
Verse 27 — Surah An-Naziat 79:27
Je, kufufuliwa kwenu, enyi watu, baada ya kufa ni kugumu zaidi, katika vipimo vyenu, au ni kuumbwa kwa mbingu
Verse 28 — Surah An-Naziat 79:28
Amezipanga juu yenu kama jengo. Na Ameinua sakafu yake angani, haina tofauti wala nyufa
Verse 29 — Surah An-Naziat 79:29
Na Ameutia giza usiku wake kwa kutwa kwa jua lake. Na Ameweka wazi mchana wake kwa kuchomoza kwake
Verse 30 — Surah An-Naziat 79:30
Na ardhi baada ya kuumba mbingu Ameitandaza. Na Ameweka humo manufaa yake
Verse 31 — Surah An-Naziat 79:31
Na Ametumbua humo chemchemu za maji. Na Ameotesha humo mimea inayolishwa
Verse 32 — Surah An-Naziat 79:32
Na Ameyakita humo majabali yakiwa ni vigingi vyake. Ameumba, Aliyetakasika na kila upungufu
Verse 33 — Surah An-Naziat 79:33
neema zote hizi zikiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu. (Hakika kurudisha kuumbwa kwenu, Siku ya Kiyama, ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kushinda kuumba viumbe hivyo vyingine. Na vyote hivyo, kwa Mwenyezi Mungu, ni rahisi na ni vipesi)
Verse 34 — Surah An-Naziat 79:34
Pindi kitakapokuja Kiyama Kikubwa na balaa nzito, nao ni Mvuvio wa pili. Kipindi hicho zitaoneshwa kwa binadamu vitendo vyake vyote, za kheri na za shari
Verse 35 — Surah An-Naziat 79:35
Hapo atazikumbuka na kuzitambua
Verse 36 — Surah An-Naziat 79:36
Na utaoneshwa Moto wa Jahanamu kwa kila aonaye, uwe waonekana waziwazi
Verse 37 — Surah An-Naziat 79:37
Ama yule atakayekiuka amri ya Mwenyezi Mungu
Verse 38 — Surah An-Naziat 79:38
na akapendelea maisha ya ulimwenguni kuliko ya Akhera
Verse 39 — Surah An-Naziat 79:39
basi kwa kweli marejeo yake ni Motoni
Verse 40 — Surah An-Naziat 79:40
Na ama yule atakayeogopa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kuhesabiwa na akaikanya nafsi yake na matamanio mapotofu
Verse 41 — Surah An-Naziat 79:41
basi Peponi ndiko makazi yake
Verse 42 — Surah An-Naziat 79:42
Wanakuuliza washirikina, ewe Mtume, kwa madharau, kuhusu wakati wa kuanzia Kiyama unachowaonya
Verse 43 — Surah An-Naziat 79:43
Wewe huna kamwe ujuzi nacho
Verse 44 — Surah An-Naziat 79:44
Bali mambo ya ujuzi huo yarejeshwe kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Sifa Tukufu
Verse 45 — Surah An-Naziat 79:45
Wewe linalokuhusu katika habari zake ni kumuonya nacho yule anayekiogopa
Verse 46 — Surah An-Naziat 79:46
Kama kwamba wao siku watakapouona Kiyama kimesimama, watakuwa hawakukaa katika maisha yao ya duniani, kwa vituko vya hiko Kiyama, isipokuwa ni kama kwamba wamkaa kati ya adhuhuri mpaka kutwa juwa, au ni kama kati ya kuchomoza jua mpaka nusu ya mchana