Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 81 - At-Takwir
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah At-Takwir 81:1
Pindi jua litakapokunjwa, na mwangaza wake ukaondoka
Verse 2 — Surah At-Takwir 81:2
Na pindi nyota zitakapopuputika na nuru yake ikafutika
Verse 3 — Surah At-Takwir 81:3
Na pindi majabali yatakapoondoshawa kwenye uso wa ardhi yakawa ni vumbi linaloenea
Verse 4 — Surah At-Takwir 81:4
Na pindi ngamia wenye mimba watakapoachwa na kupuuzwa
Verse 5 — Surah At-Takwir 81:5
Na pindi wanyama mwitu watakapokusanywa na kutangamanishwa, ili Mwenyezi Mungu Awape nafasi ya kulipizana wao kwa wao
Verse 6 — Surah At-Takwir 81:6
Na pindi bahari zitakapowashwa moto zikawa ni moto unaowaka
Verse 7 — Surah At-Takwir 81:7
Na pindi nafsi zitakapokutanishwa na mfano wake na sampuli yake
Verse 8 — Surah At-Takwir 81:8
Na pindi mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa, Siku ya Kiyama, suala la kumbembeleza na kumkejeli aliyemzika
Verse 9 — Surah At-Takwir 81:9
ni kwa dhambi gani ilikuwa kuzikwa kwake
Verse 10 — Surah At-Takwir 81:10
Na pindi kurasa za matendo zitakapoonyeshwa
Verse 11 — Surah At-Takwir 81:11
Na pindi mbingu zitakapong’olewa na kuondoshwa zilipokuwa
Verse 12 — Surah At-Takwir 81:12
Na pindi Moto utakapowashwa na ukawaka
Verse 13 — Surah At-Takwir 81:13
Na pindi Pepo , Nyumba ya Neema, itakaposongezewa watu wake wachamungu
Verse 14 — Surah At-Takwir 81:14
Litakapotokea hilo, itayakinisha kila nafsi na kujua kile ilichokitanguliza cha kheri au shari
Verse 15 — Surah At-Takwir 81:15
Anaapa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa nyota zinazofichika nuru yake mchana
Verse 16 — Surah At-Takwir 81:16
zinazotembea na zinazoghibu katika anga zake
Verse 17 — Surah At-Takwir 81:17
Na Anaapa kwa usiku unapojitokeza na giza lake
Verse 18 — Surah At-Takwir 81:18
Na kwa asubuhi unapojitokeza mwangaza wake
Verse 19 — Surah At-Takwir 81:19
Hakika Qur’ani ni ujumbe wa mjumbe mtukufu , naye ni Jibrili, amani imshukike
Verse 20 — Surah At-Takwir 81:20
Mwenye nguvu katika kuyapitisha yale anayoamrishwa. Mwenye cheo cha juu kwa Mwenyezi Mungu. Anayesikilizwa na Malaika
Verse 21 — Surah At-Takwir 81:21
Anayeaminiwa juu ya Wahyi anaoteremka nao
Verse 22 — Surah At-Takwir 81:22
Hakuwa Muhammad mnayemjua ni mwendawazimu
Verse 23 — Surah At-Takwir 81:23
Na kwa hakika Muhammad alimuona Jibrili anayemjia na utume katika pambizo kubwa
Verse 24 — Surah At-Takwir 81:24
Wala yeye hafanyi ubakhili katika kufikisha Wahyi
Verse 25 — Surah At-Takwir 81:25
Wala haikuwa hii Qur’ani ni neno la Shetani aliyefukuzwa na kutolewa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu. Lakini Qur’ani hii ni maneno ya Mwenyezi Mungu na ni Wahyi wake
Verse 26 — Surah At-Takwir 81:26
Akili zenu zawapeleka wapi katika kukanusha baada ya hoja hizi zilizo wazi na zenye nguvu
Verse 27 — Surah At-Takwir 81:27
Hayakuwa haya isipokuwa ni mawaidha kutoka kwa Mwenyezi Mungu yanapewa watu wote
Verse 28 — Surah At-Takwir 81:28
Kwa atakaye, kati yenu, kulingana juu ya haki na Imani
Verse 29 — Surah At-Takwir 81:29
Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote