Back to Languages

Swahili - Chapter 83 - Al-Mutaffifin

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Mutaffifin 83:1

Adhabu kali ni ya wale wanaopunja vipimo vya vibaba na mezani

Verse 2 — Surah Al-Mutaffifin 83:2

Ambao wakinunua kwa watu cha kupimwa kwa vibaba au kwa mizani hujikamilishia wao wenyewe

Verse 3 — Surah Al-Mutaffifin 83:3

Na wakiwauzia watu kinachouzwa kwa vibaba au mizani wanapunguza vipimo

Verse 4 — Surah Al-Mutaffifin 83:4

Basi itakuwaje hali ya yule anayeiba na kupunja katika vipimo vyote hivyo, au yule anayeiba katika vipimo hivyo na huku awapunja watu vitu vyao? Hakika huyo yuwastahiki mateso zaidi kuliko wapunguzaji wa vipimo vya vibaba na mizani. Kwani hawaamini wale wapunjaji ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kuwafufua na kuwahesabu juu ya vitendo vyao

Verse 5 — Surah Al-Mutaffifin 83:5

katika Siku itakapokuwa na kitisho

Verse 6 — Surah Al-Mutaffifin 83:6

Siku watakaposimama watu mbele ya Mweyezi Mungu ili Awahesabu kwa machache na mengi walioyatenda, hali ya kuwa wao Siku Hiyo ni wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, Mlezi wa viumbe vyote

Verse 7 — Surah Al-Mutaffifin 83:7

Hakika marejeo ya watu waovu na makazi yao yatakuwa katika hali ya dhiki

Verse 8 — Surah Al-Mutaffifin 83:8

Na ni kipi kinachokujulidha dhiki hii ni ipi

Verse 9 — Surah Al-Mutaffifin 83:9

Hakika hiyo itakuwa ni jela ya kudumu na adhabu iliyo na uchungu. Penye jela hiyo ni pale walipoandikiwa kuwa watakwenda. Wameandikiwa na imepitishwa. Hapana kitakachozidishwa wala kupunguzwa

Verse 10 — Surah Al-Mutaffifin 83:10

Adhabu kali Siku Hiyo ni ya wale wenye kukanusha

Verse 11 — Surah Al-Mutaffifin 83:11

Wale ambao wanakanusha kuwako tukio la Siku ya Malipo

Verse 12 — Surah Al-Mutaffifin 83:12

Na wala haikanushi Siku Hiyo isipokuwa kila dhalimu mwenye madhambi mengi

Verse 13 — Surah Al-Mutaffifin 83:13

Anaposomewa aya za Qur’ani, husema, «Hizi ni hadithi za urongo za watu wa kale.» Mambo yalivyo si kama wanavyodai

Verse 14 — Surah Al-Mutaffifin 83:14

Bali hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu na Wahyi Wake kwa Mtume Wake

Verse 15 — Surah Al-Mutaffifin 83:15

Na hakika zimezibwa nyoyo zao zikawa hazimkubali Mwenyezi Mungu. Na kile kilichoziziba nyoyo hizo ni kufinikwa na wingi wa madhambi wanayoyafanya. Mambo hayako kama vile wanavyodai makafiri! Bali hakika wao, Siku ya Kiyama watazibwa wasimuone Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda. Aya hii ni ushahidi kwamba Waumini watamuona Mola Wao Peponi

Verse 16 — Surah Al-Mutaffifin 83:16

Kisha hakika hao makafiri ni wenye kuingia Motoni, na wataziona na kuzihisi dharubu zake

Verse 17 — Surah Al-Mutaffifin 83:17

Kisha wataambiwa,»Haya ndiyo malipo ya yale ambayo mlikuwa mnayakanusha.»

Verse 18 — Surah Al-Mutaffifin 83:18

Ni kweli kabisa kwamba kitabu cha watu wema, nao ni wachamungu, kiko katika ngazi za juu Peponi

Verse 19 — Surah Al-Mutaffifin 83:19

Na ni kipi kinachokujulisha ni zipi hizi ngazi za juu

Verse 20 — Surah Al-Mutaffifin 83:20

Ni kitabu cha watu wema kilichopitishwa mambo yake, hakizidishwi kitu humo wala hakipunguzwi

Verse 21 — Surah Al-Mutaffifin 83:21

Wanayatazama yaliyomo ndani yake Malaika waliokurubishwa, wa kila mbingu

Verse 22 — Surah Al-Mutaffifin 83:22

Hakika wale wenye ukweli na kufuata amri za Mwenyezi Mungu watakuwa Peponi wnaneemeka

Verse 23 — Surah Al-Mutaffifin 83:23

juu ya viti vya fahari wanamwangalia Mola wao na wanaangalia yale waliyoandaliwa miongoni mwa kheri nyingi

Verse 24 — Surah Al-Mutaffifin 83:24

Unaonekana katika nyuso zao mng’aro wa neema

Verse 25 — Surah Al-Mutaffifin 83:25

Watanyweshwa tembo safi, lililotengezewa vyombo kwa ustadi na mwishowe kuna harufu ya miski

Verse 26 — Surah Al-Mutaffifin 83:26

Katika kuzipata neema hizo, nawashindane wenye kushindana

Verse 27 — Surah Al-Mutaffifin 83:27

Na kinywaji hiki, mchanganyo wake watokana na chemchemi iliyoko Peponi linalojulikana, kwa ubora wake, kwa jina la Tasnīm

Verse 28 — Surah Al-Mutaffifin 83:28

Hiyo ni chemchemi iliyoandaliwa wale waliokurubishwa kwa Mwenyezi Mungu na watajiburudisha nayo

Verse 29 — Surah Al-Mutaffifin 83:29

Hakika wale waliotenda maovu walikuwa duniani wakiwacheza shere Waumini

Verse 30 — Surah Al-Mutaffifin 83:30

Na wanapowapitia wanakonyezana kwa kuwakejeli

Verse 31 — Surah Al-Mutaffifin 83:31

Na wnaporudi, hawa waovu, kwa watu wao na jamaa zao, huwa na vihunzi na wao kwa kuwafanyia maskhara Waumini

Verse 32 — Surah Al-Mutaffifin 83:32

Na hawa makafiri wanapowaona Maswahaba wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wamefuata uongofu, huwa wakisema, «Hakika hawa wamepotea kwa kumfuata Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

Verse 33 — Surah Al-Mutaffifin 83:33

Na wala waovu hawa hawakutumwa wawe ni wachunguzi kwa Maswahaba na Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

Verse 34 — Surah Al-Mutaffifin 83:34

Basi Siku ya Kiyama wale waliomkubali Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakafanya vitendo vinavyolingana na sheria Zake, watawafanyia maskhara makafiri kama makafiri walivyokuwa wakiwafanyia mashara duniani

Verse 35 — Surah Al-Mutaffifin 83:35

Juu ya viti vya fahari, watakuwa Waumini wanaangalia yale Aliyowapa Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo matukufu na neema, wakiwa Peponi. Na neema kubwa ya zote ni kuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu

Verse 36 — Surah Al-Mutaffifin 83:36

Je, wamelipwa makafiri, pindi watakapo kufanyiwa hayo, malipo muwafaka na yale waliyoyafanya duniani ya shari na madhambi