Back to Languages

Swahili - Chapter 94 - Ash-Sharh

Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink

Verse 1 — Surah Ash-Sharh 94:1

Kwani Hatukukunjulia, ewe Mtume, kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa tabia nzuri

Verse 2 — Surah Ash-Sharh 94:2

Tukakuondolea mazito yako yaliyoemea mgongo wako

Verse 3 — Surah Ash-Sharh 94:3

na Tukakuweka, kwa matukufu Tuliyokuneemesha

Verse 4 — Surah Ash-Sharh 94:4

Verse 5 — Surah Ash-Sharh 94:5

Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa makero ya maadui zako. Kwani kwenye dhiki kuna faraji

Verse 6 — Surah Ash-Sharh 94:6

Hakika kwenye dhiki kuna faraji

Verse 7 — Surah Ash-Sharh 94:7

Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada

Verse 8 — Surah Ash-Sharh 94:8

Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako