Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 96 - Al-Alaq
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Alaq 96:1
Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba
Verse 2 — Surah Al-Alaq 96:2
Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu
Verse 3 — Surah Al-Alaq 96:3
Soma, ewe Nabii, kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu
Verse 4 — Surah Al-Alaq 96:4
Aliyewafundisha viumbe vyake kuandika kwa kalamu
Verse 5 — Surah Al-Alaq 96:5
Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu
Verse 6 — Surah Al-Alaq 96:6
Kweli, binadamu hukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu
Verse 7 — Surah Al-Alaq 96:7
akijiona ametosheka kwa utajiri wake
Verse 8 — Surah Al-Alaq 96:8
Basi, ajue kila mwenye kutupa mipaka kuwa mwisho atarudi kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Atamlipa kila binadamu kwa alilolitenda
Verse 9 — Surah Al-Alaq 96:9
Je, umeona ujeuri wa ajabu zaidi kuliko wa mtu huyu, Abu jahl
Verse 10 — Surah Al-Alaq 96:10
Anayemkataza mja wetu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, anapomsalia Mola wake
Verse 11 — Surah Al-Alaq 96:11
Waonaje iwapo mwenye kukatazwa kusali yuko uongofuni, vipi anamkataza
Verse 12 — Surah Al-Alaq 96:12
Au iwapo anaamrisha mwigine kumcha Mungu, vipi anamkataza hilo
Verse 13 — Surah Al-Alaq 96:13
Waonaje iwapo huyu mwenye kukataza anakanusha lile alinganiwalo kwalo na kulipa mgongo
Verse 14 — Surah Al-Alaq 96:14
hajui kuwa Mwenyezi Mungu anaona kila analolifanya
Verse 15 — Surah Al-Alaq 96:15
Basi mambo si kama anvyodai Abu Jahl. Na asipokomeka na ushindani alionao na udhia wake, Tutamshika upaa wake kwa nguvu na kumtia Motoni
Verse 16 — Surah Al-Alaq 96:16
Upaa wake ni upaa wenye maneno ya urongo na vitendo vya makosa
Verse 17 — Surah Al-Alaq 96:17
Basi na awalete, mtupaji mipaka huyu, watu wa baraza ili wamsaidiye
Verse 18 — Surah Al-Alaq 96:18
Sisi Tutawaita Malaika wa adhabu
Verse 19 — Surah Al-Alaq 96:19
Mambo si kama Abu Jahl anavyoyadhania. Yeye, ewe Mtume, hawezi kukufanya lolote la kukudhuru Usimfuate kwa lile alilokuitia la kuwa uache Swala, bali msujudie Mola wako na uwe karibu na Yeye kwa kujipendekeza Kwake kwa kumtii