Verse 1 — Surah Al-Fatiha 1:1
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Verse 2 — Surah Al-Fatiha 1:2
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote
Verse 3 — Surah Al-Fatiha 1:3
Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Verse 4 — Surah Al-Fatiha 1:4
Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo
Verse 5 — Surah Al-Fatiha 1:5
Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada
Verse 6 — Surah Al-Fatiha 1:6
Tuongoe njia iliyo nyooka
Verse 7 — Surah Al-Fatiha 1:7
Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea