Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 110 - An-Nasr
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah An-Nasr 110:1
Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi
Verse 2 — Surah An-Nasr 110:2
Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi
Verse 3 — Surah An-Nasr 110:3
Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba