Back to Languages

Swahili - Chapter 3 - Al-Imran

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 153 — Surah Al-Imran 3:153

Pale mlipo kuwa mkikimbia mbio wala hamumsikilizi yeyote, na Mtume anakuiteni, yuko nyuma yenu. Mwenyezi Mungu akakupeni dhiki juu ya dhiki, ili msisikitike kwa yaliyo kukoseeni wala kwa yaliyo kusibuni. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda