Back to Languages

Swahili - Chapter 30 - Ar-Rum

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 28 — Surah Ar-Rum 30:28

Amekupigieni mfano kutokana na nafsi zenu. Je! Katika hao iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyo kuruzukuni, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyo ogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivi tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye akili