Back to Languages

Swahili - Chapter 30 - Ar-Rum

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Ar-Rum 30:1

Alif Lam Mim (A. L. M)

Verse 2 — Surah Ar-Rum 30:2

Verse 3 — Surah Ar-Rum 30:3

Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda

Verse 4 — Surah Ar-Rum 30:4

Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi

Verse 5 — Surah Ar-Rum 30:5

Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 6 — Surah Ar-Rum 30:6

Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui

Verse 7 — Surah Ar-Rum 30:7

Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera

Verse 8 — Surah Ar-Rum 30:8

Je! Hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake ila kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi

Verse 9 — Surah Ar-Rum 30:9

Je! Hawatembei katika ardhi wakaona ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyo istawisha wao. Na Mitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao

Verse 10 — Surah Ar-Rum 30:10

Kisha ulikuwa mwisho wa walio fanya ubaya ni kuzikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawa wanazifanyia maskhara

Verse 11 — Surah Ar-Rum 30:11

Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake

Verse 12 — Surah Ar-Rum 30:12

Na itapo simama Saa wakosefu watakata tamaa

Verse 13 — Surah Ar-Rum 30:13

Wala hawatakuwa na waombezi miongoni mwa walio kuwa wakiwashirikisha na Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao

Verse 14 — Surah Ar-Rum 30:14

Na siku itapo simama Saa, siku hiyo watagawanyika

Verse 15 — Surah Ar-Rum 30:15

Ama walio amini na wakatenda mema watafurahishwa katika Bustani

Verse 16 — Surah Ar-Rum 30:16

Na ama walio kufuru na wakazikanusha Ishara zetu na mkutano wa Akhera, hao basi watahudhurishwa katika adhabu

Verse 17 — Surah Ar-Rum 30:17

Basi Subhanallah! Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni na asubuhi

Verse 18 — Surah Ar-Rum 30:18

Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri

Verse 19 — Surah Ar-Rum 30:19

Hukitoa kilicho hai kutokana na kilicho kufa, na hukitoa kilicho kufa kutokana na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo mtavyo fufuliwa

Verse 20 — Surah Ar-Rum 30:20

Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote

Verse 21 — Surah Ar-Rum 30:21

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri

Verse 22 — Surah Ar-Rum 30:22

Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi

Verse 23 — Surah Ar-Rum 30:23

Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao sikia

Verse 24 — Surah Ar-Rum 30:24

Na katika Ishara zake hukuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na tamaa. Na hukuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao zingatia

Verse 25 — Surah Ar-Rum 30:25

Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapo kuiteni mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi

Verse 26 — Surah Ar-Rum 30:26

Na vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamt'ii Yeye

Verse 27 — Surah Ar-Rum 30:27

Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima

Verse 28 — Surah Ar-Rum 30:28

Amekupigieni mfano kutokana na nafsi zenu. Je! Katika hao iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyo kuruzukuni, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyo ogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivi tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye akili

Verse 29 — Surah Ar-Rum 30:29

Bali walio dhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha apotee? Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru

Verse 30 — Surah Ar-Rum 30:30

Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui

Verse 31 — Surah Ar-Rum 30:31

Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na shikeni Sala, na wala msiwe katika washirikina

Verse 32 — Surah Ar-Rum 30:32

Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho

Verse 33 — Surah Ar-Rum 30:33

Yakiwapata watu madhara humwomba Mola wao Mlezi nao wametubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola wao Mlezi

Verse 34 — Surah Ar-Rum 30:34

Kwa kuyakataa tuliyo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua

Verse 35 — Surah Ar-Rum 30:35

Au tumewateremshia hoja ambayo kwayo ndio wanafanya ushirikina

Verse 36 — Surah Ar-Rum 30:36

Na watu tunapo waonjesha rehema huifurahia, na ukiwasibu uovu kwa iliyo yatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa

Verse 37 — Surah Ar-Rum 30:37

Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye? Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini

Verse 38 — Surah Ar-Rum 30:38

Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni kheri kwa watakao radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa

Verse 39 — Surah Ar-Rum 30:39

Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watao zidishiwa

Verse 40 — Surah Ar-Rum 30:40

Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika hao mnao washirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo mshirikisha naye

Verse 41 — Surah Ar-Rum 30:41

Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu

Verse 42 — Surah Ar-Rum 30:42

Sema: Safirini duniani muangalie ulikuwaje mwisho wa walio tangulia. Wengi wao walikuwa washirikina

Verse 43 — Surah Ar-Rum 30:43

Basi uelekeze uso wako kwenye Dini Iliyo Nyooka kabla ya kufika Siku hiyo isiyo zuilika, inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu watatengana

Verse 44 — Surah Ar-Rum 30:44

Anaye kufuru basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe, na anaye tenda mema, basi wanazitengezea nafsi zao

Verse 45 — Surah Ar-Rum 30:45

Ili awalipe walio amini na wakatenda mema kutokana na fadhila yake. Hakika Yeye hawapendi makafiri

Verse 46 — Surah Ar-Rum 30:46

Na katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara njema, na ili kukuonjesheni baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yende kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru

Verse 47 — Surah Ar-Rum 30:47

Na hakika tulikwisha watuma Mitume kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale walio fanya ukosefu. Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini

Verse 48 — Surah Ar-Rum 30:48

Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapo wafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha

Verse 49 — Surah Ar-Rum 30:49

Na ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa

Verse 50 — Surah Ar-Rum 30:50

Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyo ihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo ndiye bila ya shaka Mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu

Verse 51 — Surah Ar-Rum 30:51

Na tunge utuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya manjano, juu ya hayo wange endelea kukufuru

Verse 52 — Surah Ar-Rum 30:52

Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala viziwi wakasikia wito wakisha geuka kukupa mgongo

Verse 53 — Surah Ar-Rum 30:53

Wala wewe huwaongoi vipofu na upotovu wao. Huwasikilizishi ila wanao ziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walio nyenyekea

Verse 54 — Surah Ar-Rum 30:54

Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza

Verse 55 — Surah Ar-Rum 30:55

Na siku itapo simama Saa wakosefu wataapa kwamba hawakukaa duniani ila saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyo kuwa wakipotozwa

Verse 56 — Surah Ar-Rum 30:56

Na walio pewa ilimu na Imani watasema: Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui

Verse 57 — Surah Ar-Rum 30:57

Basi Siku hiyo hautawafaa walio dhulumu udhuru wao, wala haitotakiwa toba yao

Verse 58 — Surah Ar-Rum 30:58

Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika hii Qur'ani. Na ukiwaletea Ishara yoyote hapana shaka walio kufuru watasema: Nyinyi si chochote ila ni waongo

Verse 59 — Surah Ar-Rum 30:59

Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga muhuri kwenye nyoyo za wasio jua

Verse 60 — Surah Ar-Rum 30:60

Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Wala wasikupaparishe hao wasio kuwa na yakini