Back to Languages

Swahili - Chapter 35 - Fatir

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Fatir 35:1

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili-mbili, na tatu- tatu, na nne-nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu