Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 36 - Ya-Sin
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Ya-Sin 36:1
Ya-Sin (Y. S)
Verse 2 — Surah Ya-Sin 36:2
Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima
Verse 3 — Surah Ya-Sin 36:3
Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa
Verse 4 — Surah Ya-Sin 36:4
Juu ya Njia Iliyo Nyooka
Verse 5 — Surah Ya-Sin 36:5
Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu
Verse 6 — Surah Ya-Sin 36:6
Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika
Verse 7 — Surah Ya-Sin 36:7
Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini
Verse 8 — Surah Ya-Sin 36:8
Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu
Verse 9 — Surah Ya-Sin 36:9
Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni
Verse 10 — Surah Ya-Sin 36:10
Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini
Verse 11 — Surah Ya-Sin 36:11
Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema
Verse 12 — Surah Ya-Sin 36:12
Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha
Verse 13 — Surah Ya-Sin 36:13
Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa
Verse 14 — Surah Ya-Sin 36:14
Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu
Verse 15 — Surah Ya-Sin 36:15
Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu
Verse 16 — Surah Ya-Sin 36:16
Wakasema: Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu
Verse 17 — Surah Ya-Sin 36:17
Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi
Verse 18 — Surah Ya-Sin 36:18
Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu
Verse 19 — Surah Ya-Sin 36:19
Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka
Verse 20 — Surah Ya-Sin 36:20
Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa walio tumwa
Verse 21 — Surah Ya-Sin 36:21
Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka
Verse 22 — Surah Ya-Sin 36:22
NA KWA NINI nisimuabudu yule aliye niumba na kwake mtarejeshwa
Verse 23 — Surah Ya-Sin 36:23
Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa
Verse 24 — Surah Ya-Sin 36:24
Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri
Verse 25 — Surah Ya-Sin 36:25
Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni
Verse 26 — Surah Ya-Sin 36:26
Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua
Verse 27 — Surah Ya-Sin 36:27
Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, na akanifanya miongoni mwa walio hishimiwa
Verse 28 — Surah Ya-Sin 36:28
Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha
Verse 29 — Surah Ya-Sin 36:29
Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa
Verse 30 — Surah Ya-Sin 36:30
Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli
Verse 31 — Surah Ya-Sin 36:31
Je! Hawaoni umma ngapi tulizo ziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao
Verse 32 — Surah Ya-Sin 36:32
Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu
Verse 33 — Surah Ya-Sin 36:33
Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila
Verse 34 — Surah Ya-Sin 36:34
Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake
Verse 35 — Surah Ya-Sin 36:35
Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru
Verse 36 — Surah Ya-Sin 36:36
Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua
Verse 37 — Surah Ya-Sin 36:37
Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani
Verse 38 — Surah Ya-Sin 36:38
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua
Verse 39 — Surah Ya-Sin 36:39
Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe
Verse 40 — Surah Ya-Sin 36:40
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao
Verse 41 — Surah Ya-Sin 36:41
Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni
Verse 42 — Surah Ya-Sin 36:42
Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyo vipanda
Verse 43 — Surah Ya-Sin 36:43
Na tukitaka tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi
Verse 44 — Surah Ya-Sin 36:44
Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda
Verse 45 — Surah Ya-Sin 36:45
Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa
Verse 46 — Surah Ya-Sin 36:46
Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza
Verse 47 — Surah Ya-Sin 36:47
Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeni Mwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini: Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhaahiri
Verse 48 — Surah Ya-Sin 36:48
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli
Verse 49 — Surah Ya-Sin 36:49
Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana
Verse 50 — Surah Ya-Sin 36:50
Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei
Verse 51 — Surah Ya-Sin 36:51
Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi
Verse 52 — Surah Ya-Sin 36:52
Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume
Verse 53 — Surah Ya-Sin 36:53
Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu
Verse 54 — Surah Ya-Sin 36:54
Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda
Verse 55 — Surah Ya-Sin 36:55
Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi
Verse 56 — Surah Ya-Sin 36:56
Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari
Verse 57 — Surah Ya-Sin 36:57
Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka
Verse 58 — Surah Ya-Sin 36:58
Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu
Verse 59 — Surah Ya-Sin 36:59
Na enyi wakosefu! Jitengeni leo
Verse 60 — Surah Ya-Sin 36:60
Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu
Verse 61 — Surah Ya-Sin 36:61
Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka
Verse 62 — Surah Ya-Sin 36:62
Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri
Verse 63 — Surah Ya-Sin 36:63
Hii basi ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa
Verse 64 — Surah Ya-Sin 36:64
Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru
Verse 65 — Surah Ya-Sin 36:65
Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma
Verse 66 — Surah Ya-Sin 36:66
Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje
Verse 67 — Surah Ya-Sin 36:67
Na tungeli taka tunge wageuza sura hapo hapo walipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi
Verse 68 — Surah Ya-Sin 36:68
Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii
Verse 69 — Surah Ya-Sin 36:69
Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha
Verse 70 — Surah Ya-Sin 36:70
Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri
Verse 71 — Surah Ya-Sin 36:71
Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki
Verse 72 — Surah Ya-Sin 36:72
Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao wapanda, na baadhi yao wanawala
Verse 73 — Surah Ya-Sin 36:73
Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru
Verse 74 — Surah Ya-Sin 36:74
Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa
Verse 75 — Surah Ya-Sin 36:75
Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa
Verse 76 — Surah Ya-Sin 36:76
Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaweka siri na wanayo yatangaza
Verse 77 — Surah Ya-Sin 36:77
Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri
Verse 78 — Surah Ya-Sin 36:78
Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika
Verse 79 — Surah Ya-Sin 36:79
Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba
Verse 80 — Surah Ya-Sin 36:80
Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha
Verse 81 — Surah Ya-Sin 36:81
Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi
Verse 82 — Surah Ya-Sin 36:82
Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa
Verse 83 — Surah Ya-Sin 36:83
Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa