Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 37 - As-Saffat
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah As-Saffat 37:1
Naapa kwa wanao jipanga kwa safu
Verse 2 — Surah As-Saffat 37:2
Na kwa wenye kukataza mabaya
Verse 3 — Surah As-Saffat 37:3
Na kwa wenye kusoma Ukumbusho
Verse 4 — Surah As-Saffat 37:4
Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja
Verse 5 — Surah As-Saffat 37:5
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote
Verse 6 — Surah As-Saffat 37:6
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota
Verse 7 — Surah As-Saffat 37:7
Na kulinda na kila shet'ani a'si
Verse 8 — Surah As-Saffat 37:8
Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande
Verse 9 — Surah As-Saffat 37:9
Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu
Verse 10 — Surah As-Saffat 37:10
Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara
Verse 11 — Surah As-Saffat 37:11
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata
Verse 12 — Surah As-Saffat 37:12
Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara
Verse 13 — Surah As-Saffat 37:13
Na wanapo kumbushwa hawakumbuki
Verse 14 — Surah As-Saffat 37:14
Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara
Verse 15 — Surah As-Saffat 37:15
Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri
Verse 16 — Surah As-Saffat 37:16
Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa
Verse 17 — Surah As-Saffat 37:17
Hata baba zetu wa zamani
Verse 18 — Surah As-Saffat 37:18
Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili
Verse 19 — Surah As-Saffat 37:19
Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona
Verse 20 — Surah As-Saffat 37:20
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo
Verse 21 — Surah As-Saffat 37:21
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha
Verse 22 — Surah As-Saffat 37:22
Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu
Verse 23 — Surah As-Saffat 37:23
Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu
Verse 24 — Surah As-Saffat 37:24
Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa
Verse 25 — Surah As-Saffat 37:25
Mna nini? Mbona hamsaidiani
Verse 26 — Surah As-Saffat 37:26
Bali hii leo, watasalimu amri
Verse 27 — Surah As-Saffat 37:27
Watakabiliana wao kwa wao kuulizana
Verse 28 — Surah As-Saffat 37:28
Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia
Verse 29 — Surah As-Saffat 37:29
Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini
Verse 30 — Surah As-Saffat 37:30
Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu
Verse 31 — Surah As-Saffat 37:31
Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu
Verse 32 — Surah As-Saffat 37:32
Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu
Verse 33 — Surah As-Saffat 37:33
Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja
Verse 34 — Surah As-Saffat 37:34
Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu
Verse 35 — Surah As-Saffat 37:35
Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna
Verse 36 — Surah As-Saffat 37:36
Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu
Verse 37 — Surah As-Saffat 37:37
Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume
Verse 38 — Surah As-Saffat 37:38
Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu
Verse 39 — Surah As-Saffat 37:39
Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya
Verse 40 — Surah As-Saffat 37:40
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa
Verse 41 — Surah As-Saffat 37:41
Hao ndio watakao pata riziki maalumu
Verse 42 — Surah As-Saffat 37:42
Matunda, nao watahishimiwa
Verse 43 — Surah As-Saffat 37:43
Katika Bustani za neema
Verse 44 — Surah As-Saffat 37:44
Wako juu ya viti wamekabiliana
Verse 45 — Surah As-Saffat 37:45
Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem
Verse 46 — Surah As-Saffat 37:46
Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao
Verse 47 — Surah As-Saffat 37:47
Hakina madhara, wala hakiwaleweshi
Verse 48 — Surah As-Saffat 37:48
Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri
Verse 49 — Surah As-Saffat 37:49
Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika
Verse 50 — Surah As-Saffat 37:50
Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe
Verse 51 — Surah As-Saffat 37:51
Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki
Verse 52 — Surah As-Saffat 37:52
Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki
Verse 53 — Surah As-Saffat 37:53
Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa
Verse 54 — Surah As-Saffat 37:54
Atasema: Je! Nyie mnawaona
Verse 55 — Surah As-Saffat 37:55
Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu
Verse 56 — Surah As-Saffat 37:56
Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza
Verse 57 — Surah As-Saffat 37:57
Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa
Verse 58 — Surah As-Saffat 37:58
Je! Sisi hatutakufa
Verse 59 — Surah As-Saffat 37:59
Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa
Verse 60 — Surah As-Saffat 37:60
Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa
Verse 61 — Surah As-Saffat 37:61
Kwa mfano wa haya nawatende watendao
Verse 62 — Surah As-Saffat 37:62
Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum
Verse 63 — Surah As-Saffat 37:63
Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu
Verse 64 — Surah As-Saffat 37:64
Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu
Verse 65 — Surah As-Saffat 37:65
Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani
Verse 66 — Surah As-Saffat 37:66
Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo
Verse 67 — Surah As-Saffat 37:67
Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka
Verse 68 — Surah As-Saffat 37:68
Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu
Verse 69 — Surah As-Saffat 37:69
Hakika waliwakuta baba zao wamepotea
Verse 70 — Surah As-Saffat 37:70
Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao
Verse 71 — Surah As-Saffat 37:71
Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani
Verse 72 — Surah As-Saffat 37:72
Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji
Verse 73 — Surah As-Saffat 37:73
Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa
Verse 74 — Surah As-Saffat 37:74
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa
Verse 75 — Surah As-Saffat 37:75
Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji
Verse 76 — Surah As-Saffat 37:76
Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa
Verse 77 — Surah As-Saffat 37:77
Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia
Verse 78 — Surah As-Saffat 37:78
Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye
Verse 79 — Surah As-Saffat 37:79
Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote
Verse 80 — Surah As-Saffat 37:80
Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema
Verse 81 — Surah As-Saffat 37:81
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini
Verse 82 — Surah As-Saffat 37:82
Kisha tukawazamisha wale wengine
Verse 83 — Surah As-Saffat 37:83
Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake
Verse 84 — Surah As-Saffat 37:84
Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima
Verse 85 — Surah As-Saffat 37:85
Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini
Verse 86 — Surah As-Saffat 37:86
Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu
Verse 87 — Surah As-Saffat 37:87
Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote
Verse 88 — Surah As-Saffat 37:88
Kisha akapiga jicho kutazama nyota
Verse 89 — Surah As-Saffat 37:89
Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa
Verse 90 — Surah As-Saffat 37:90
Nao wakamwacha, wakampa kisogo
Verse 91 — Surah As-Saffat 37:91
Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli
Verse 92 — Surah As-Saffat 37:92
Mna nini hata hamsemi
Verse 93 — Surah As-Saffat 37:93
Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia
Verse 94 — Surah As-Saffat 37:94
Basi wakamjia upesi upesi
Verse 95 — Surah As-Saffat 37:95
Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe
Verse 96 — Surah As-Saffat 37:96
Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya
Verse 97 — Surah As-Saffat 37:97
Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo
Verse 98 — Surah As-Saffat 37:98
Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini
Verse 99 — Surah As-Saffat 37:99
Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa
Verse 100 — Surah As-Saffat 37:100
Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema
Verse 101 — Surah As-Saffat 37:101
Basi tukambashiria mwana aliye mpole
Verse 102 — Surah As-Saffat 37:102
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri
Verse 103 — Surah As-Saffat 37:103
Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji
Verse 104 — Surah As-Saffat 37:104
Tulimwita: Ewe Ibrahim
Verse 105 — Surah As-Saffat 37:105
Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema
Verse 106 — Surah As-Saffat 37:106
Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri
Verse 107 — Surah As-Saffat 37:107
Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu
Verse 108 — Surah As-Saffat 37:108
Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye
Verse 109 — Surah As-Saffat 37:109
Iwe salama kwa Ibrahim
Verse 110 — Surah As-Saffat 37:110
Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema
Verse 111 — Surah As-Saffat 37:111
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini
Verse 112 — Surah As-Saffat 37:112
Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema
Verse 113 — Surah As-Saffat 37:113
Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi
Verse 114 — Surah As-Saffat 37:114
Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni
Verse 115 — Surah As-Saffat 37:115
Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa
Verse 116 — Surah As-Saffat 37:116
Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda
Verse 117 — Surah As-Saffat 37:117
Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha
Verse 118 — Surah As-Saffat 37:118
Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka
Verse 119 — Surah As-Saffat 37:119
Na tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye
Verse 120 — Surah As-Saffat 37:120
Iwe salama kwa Musa na Haruni
Verse 121 — Surah As-Saffat 37:121
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema
Verse 122 — Surah As-Saffat 37:122
Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini
Verse 123 — Surah As-Saffat 37:123
Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume
Verse 124 — Surah As-Saffat 37:124
Alipo waambia watu wake: Hamwogopi
Verse 125 — Surah As-Saffat 37:125
Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji
Verse 126 — Surah As-Saffat 37:126
Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani
Verse 127 — Surah As-Saffat 37:127
Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa
Verse 128 — Surah As-Saffat 37:128
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa
Verse 129 — Surah As-Saffat 37:129
Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye
Verse 130 — Surah As-Saffat 37:130
Iwe salama kwa Ilyas
Verse 131 — Surah As-Saffat 37:131
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema
Verse 132 — Surah As-Saffat 37:132
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini
Verse 133 — Surah As-Saffat 37:133
Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume
Verse 134 — Surah As-Saffat 37:134
Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote
Verse 135 — Surah As-Saffat 37:135
Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma
Verse 136 — Surah As-Saffat 37:136
Kisha tukawaangamiza wale wengineo
Verse 137 — Surah As-Saffat 37:137
Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi
Verse 138 — Surah As-Saffat 37:138
Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini
Verse 139 — Surah As-Saffat 37:139
Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume
Verse 140 — Surah As-Saffat 37:140
Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni
Verse 141 — Surah As-Saffat 37:141
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa
Verse 142 — Surah As-Saffat 37:142
Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa
Verse 143 — Surah As-Saffat 37:143
Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu
Verse 144 — Surah As-Saffat 37:144
Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa
Verse 145 — Surah As-Saffat 37:145
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa
Verse 146 — Surah As-Saffat 37:146
Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye
Verse 147 — Surah As-Saffat 37:147
Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi
Verse 148 — Surah As-Saffat 37:148
Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda
Verse 149 — Surah As-Saffat 37:149
Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume
Verse 150 — Surah As-Saffat 37:150
Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia
Verse 151 — Surah As-Saffat 37:151
Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema
Verse 152 — Surah As-Saffat 37:152
Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo
Verse 153 — Surah As-Saffat 37:153
Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume
Verse 154 — Surah As-Saffat 37:154
Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi
Verse 155 — Surah As-Saffat 37:155
Hamkumbuki
Verse 156 — Surah As-Saffat 37:156
Au mnayo hoja iliyo wazi
Verse 157 — Surah As-Saffat 37:157
Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli
Verse 158 — Surah As-Saffat 37:158
Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa
Verse 159 — Surah As-Saffat 37:159
Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia
Verse 160 — Surah As-Saffat 37:160
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa
Verse 161 — Surah As-Saffat 37:161
Basi hakika nyinyi na mnao waabudu
Verse 162 — Surah As-Saffat 37:162
Hamwezi kuwapoteza
Verse 163 — Surah As-Saffat 37:163
Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni
Verse 164 — Surah As-Saffat 37:164
Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu
Verse 165 — Surah As-Saffat 37:165
Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu
Verse 166 — Surah As-Saffat 37:166
Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa
Verse 167 — Surah As-Saffat 37:167
Na walikuwapo walio kuwa wakisema
Verse 168 — Surah As-Saffat 37:168
Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani
Verse 169 — Surah As-Saffat 37:169
Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi
Verse 170 — Surah As-Saffat 37:170
Lakini waliukataa. Basi watakuja jua
Verse 171 — Surah As-Saffat 37:171
Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa
Verse 172 — Surah As-Saffat 37:172
Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa
Verse 173 — Surah As-Saffat 37:173
Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda
Verse 174 — Surah As-Saffat 37:174
Basi waachilie mbali kwa muda
Verse 175 — Surah As-Saffat 37:175
Na watazame, nao wataona
Verse 176 — Surah As-Saffat 37:176
Je! Wanaihimiza adhabu yetu
Verse 177 — Surah As-Saffat 37:177
Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa
Verse 178 — Surah As-Saffat 37:178
Na waache kwa muda
Verse 179 — Surah As-Saffat 37:179
Na tazama, na wao wataona
Verse 180 — Surah As-Saffat 37:180
Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia
Verse 181 — Surah As-Saffat 37:181
Na Salamu juu ya Mitume
Verse 182 — Surah As-Saffat 37:182
Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote