Back to Languages

Swahili - Chapter 38 - Sad

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Sad 38:1

S'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha

Verse 2 — Surah Sad 38:2

Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani

Verse 3 — Surah Sad 38:3

Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita

Verse 4 — Surah Sad 38:4

Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo

Verse 5 — Surah Sad 38:5

Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu

Verse 6 — Surah Sad 38:6

Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa

Verse 7 — Surah Sad 38:7

Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu

Verse 8 — Surah Sad 38:8

Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu

Verse 9 — Surah Sad 38:9

Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji

Verse 10 — Surah Sad 38:10

Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko

Verse 11 — Surah Sad 38:11

Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa

Verse 12 — Surah Sad 38:12

Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo

Verse 13 — Surah Sad 38:13

Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi

Verse 14 — Surah Sad 38:14

Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu

Verse 15 — Surah Sad 38:15

Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda

Verse 16 — Surah Sad 38:16

Na wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hisabu

Verse 17 — Surah Sad 38:17

Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia

Verse 18 — Surah Sad 38:18

Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye

Verse 19 — Surah Sad 38:19

Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake

Verse 20 — Surah Sad 38:20

Na tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hikima, na kukata hukumu

Verse 21 — Surah Sad 38:21

Na je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani

Verse 22 — Surah Sad 38:22

Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa

Verse 23 — Surah Sad 38:23

Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisiini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno

Verse 24 — Surah Sad 38:24

Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia

Verse 25 — Surah Sad 38:25

Basi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu

Verse 26 — Surah Sad 38:26

Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu

Verse 27 — Surah Sad 38:27

Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata

Verse 28 — Surah Sad 38:28

Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu

Verse 29 — Surah Sad 38:29

Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili

Verse 30 — Surah Sad 38:30

Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia

Verse 31 — Surah Sad 38:31

Alipo pelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti

Verse 32 — Surah Sad 38:32

Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma

Verse 33 — Surah Sad 38:33

(Akasema:) Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo

Verse 34 — Surah Sad 38:34

Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu

Verse 35 — Surah Sad 38:35

Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji

Verse 36 — Surah Sad 38:36

Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika

Verse 37 — Surah Sad 38:37

Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi

Verse 38 — Surah Sad 38:38

Na wengine wafungwao kwa minyororo

Verse 39 — Surah Sad 38:39

Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu

Verse 40 — Surah Sad 38:40

Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea

Verse 41 — Surah Sad 38:41

Na mkumbuke mja wetu Ayubu alipo mwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika Shet'ani amenifikishia udhia na adhabu

Verse 42 — Surah Sad 38:42

(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa

Verse 43 — Surah Sad 38:43

Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili

Verse 44 — Surah Sad 38:44

Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu

Verse 45 — Surah Sad 38:45

Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu walio kuwa na nguvu na busara

Verse 46 — Surah Sad 38:46

Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera

Verse 47 — Surah Sad 38:47

Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora

Verse 48 — Surah Sad 38:48

Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora

Verse 49 — Surah Sad 38:49

Huu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri

Verse 50 — Surah Sad 38:50

Bustani za milele zitazo funguliwa milango yao kwa ajili yao

Verse 51 — Surah Sad 38:51

Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji

Verse 52 — Surah Sad 38:52

Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao

Verse 53 — Surah Sad 38:53

Haya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu

Verse 54 — Surah Sad 38:54

Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika

Verse 55 — Surah Sad 38:55

Ndio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa

Verse 56 — Surah Sad 38:56

Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia

Verse 57 — Surah Sad 38:57

Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha

Verse 58 — Surah Sad 38:58

Na adhabu nyenginezo za namna hii

Verse 59 — Surah Sad 38:59

Hili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni

Verse 60 — Surah Sad 38:60

Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya, napo ni pahala paovu kabisa

Verse 61 — Surah Sad 38:61

Waseme: Mola wetu Mlezi! Aliye tusabibisha haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni

Verse 62 — Surah Sad 38:62

Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu

Verse 63 — Surah Sad 38:63

Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni

Verse 64 — Surah Sad 38:64

Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni

Verse 65 — Surah Sad 38:65

Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu

Verse 66 — Surah Sad 38:66

Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe

Verse 67 — Surah Sad 38:67

Sema: Hii ni khabari kubwa kabisa

Verse 68 — Surah Sad 38:68

Ambayo nyinyi mnaipuuza

Verse 69 — Surah Sad 38:69

Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana

Verse 70 — Surah Sad 38:70

Haikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhaahiri

Verse 71 — Surah Sad 38:71

Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo

Verse 72 — Surah Sad 38:72

Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii

Verse 73 — Surah Sad 38:73

Basi Malaika wakat'ii wote pamoja

Verse 74 — Surah Sad 38:74

Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri

Verse 75 — Surah Sad 38:75

Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli

Verse 76 — Surah Sad 38:76

Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo

Verse 77 — Surah Sad 38:77

Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika

Verse 78 — Surah Sad 38:78

Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo

Verse 79 — Surah Sad 38:79

Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe

Verse 80 — Surah Sad 38:80

Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula

Verse 81 — Surah Sad 38:81

Mpaka siku ya wakati maalumu

Verse 82 — Surah Sad 38:82

Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote

Verse 83 — Surah Sad 38:83

Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa

Verse 84 — Surah Sad 38:84

Akasema: Haki! Na haki ninaisema

Verse 85 — Surah Sad 38:85

Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao

Verse 86 — Surah Sad 38:86

Sema (Ewe Mtume): Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu

Verse 87 — Surah Sad 38:87

Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote

Verse 88 — Surah Sad 38:88

Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda