Back to Languages

Swahili - Chapter 35 - Fatir

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 45 — Surah Fatir 35:45

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa waliyo yachuma, basi asingeli muacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara