Back to Languages

Swahili - Chapter 4 - An-Nisa

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 59 — Surah An-Nisa 4:59

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema