Back to Languages

Swahili - Chapter 4 - An-Nisa

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 81 — Surah An-Nisa 4:81

Na wanasema: Tunat'ii. Lakini wanapo toka kwako kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayo yasema. Na Mwenyezi Mungu anayaandika yote hayo wanayo yapangia njama za usiku. Basi waachilie mbali, na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha