Back to Languages

Swahili - Chapter 42 - Ash-Shura

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 45 — Surah Ash-Shura 42:45

Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto, nao wamenyenyekea kwa unyonge, wanatazama kwa mtazamo wa kificho. Na walio amini watasema: Hakika wapatao khasara ni hao walio khasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Ama hakika wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya daima