Back to Languages

Swahili - Chapter 5 - Al-Maidah

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Maidah 5:1

Enyi mlio amini! Timizeni ahadi. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo, ila wale mnao tajiwa. Lakini msihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Hija. Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu apendavyo