Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 55 - Ar-Rahman
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Ar-Rahman 55:1
Arrah'man, Mwingi wa Rehema
Verse 2 — Surah Ar-Rahman 55:2
Amefundisha Qur'ani
Verse 3 — Surah Ar-Rahman 55:3
Amemuumba mwanaadamu
Verse 4 — Surah Ar-Rahman 55:4
Akamfundisha kubaini
Verse 5 — Surah Ar-Rahman 55:5
Jua na mwezi huenda kwa hisabu
Verse 6 — Surah Ar-Rahman 55:6
Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea
Verse 7 — Surah Ar-Rahman 55:7
Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani
Verse 8 — Surah Ar-Rahman 55:8
Ili msidhulumu katika mizani
Verse 9 — Surah Ar-Rahman 55:9
Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani
Verse 10 — Surah Ar-Rahman 55:10
Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe
Verse 11 — Surah Ar-Rahman 55:11
Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba
Verse 12 — Surah Ar-Rahman 55:12
Na nafaka zenye makapi, na rehani
Verse 13 — Surah Ar-Rahman 55:13
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 14 — Surah Ar-Rahman 55:14
Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo
Verse 15 — Surah Ar-Rahman 55:15
Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto
Verse 16 — Surah Ar-Rahman 55:16
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 17 — Surah Ar-Rahman 55:17
Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili
Verse 18 — Surah Ar-Rahman 55:18
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 19 — Surah Ar-Rahman 55:19
Anaziendesha bahari mbili zikutane
Verse 20 — Surah Ar-Rahman 55:20
Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane
Verse 21 — Surah Ar-Rahman 55:21
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 22 — Surah Ar-Rahman 55:22
Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani
Verse 23 — Surah Ar-Rahman 55:23
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 24 — Surah Ar-Rahman 55:24
Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima
Verse 25 — Surah Ar-Rahman 55:25
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 26 — Surah Ar-Rahman 55:26
Kila kilioko juu yake kitatoweka
Verse 27 — Surah Ar-Rahman 55:27
Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu
Verse 28 — Surah Ar-Rahman 55:28
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 29 — Surah Ar-Rahman 55:29
Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo
Verse 30 — Surah Ar-Rahman 55:30
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 31 — Surah Ar-Rahman 55:31
Tutakuhisabuni enyi makundi mawili
Verse 32 — Surah Ar-Rahman 55:32
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 33 — Surah Ar-Rahman 55:33
Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka
Verse 34 — Surah Ar-Rahman 55:34
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 35 — Surah Ar-Rahman 55:35
Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda
Verse 36 — Surah Ar-Rahman 55:36
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 37 — Surah Ar-Rahman 55:37
Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta
Verse 38 — Surah Ar-Rahman 55:38
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 39 — Surah Ar-Rahman 55:39
Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini
Verse 40 — Surah Ar-Rahman 55:40
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 41 — Surah Ar-Rahman 55:41
Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu
Verse 42 — Surah Ar-Rahman 55:42
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 43 — Surah Ar-Rahman 55:43
Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha
Verse 44 — Surah Ar-Rahman 55:44
Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka
Verse 45 — Surah Ar-Rahman 55:45
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 46 — Surah Ar-Rahman 55:46
Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili
Verse 47 — Surah Ar-Rahman 55:47
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 48 — Surah Ar-Rahman 55:48
Bustani zenye matawi yaliyo tanda
Verse 49 — Surah Ar-Rahman 55:49
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 50 — Surah Ar-Rahman 55:50
Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita
Verse 51 — Surah Ar-Rahman 55:51
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 52 — Surah Ar-Rahman 55:52
Humo katika kila matunda zimo namna mbili
Verse 53 — Surah Ar-Rahman 55:53
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 54 — Surah Ar-Rahman 55:54
Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu
Verse 55 — Surah Ar-Rahman 55:55
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 56 — Surah Ar-Rahman 55:56
Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini
Verse 57 — Surah Ar-Rahman 55:57
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 58 — Surah Ar-Rahman 55:58
Kama kwamba wao ni yakuti na marijani
Verse 59 — Surah Ar-Rahman 55:59
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 60 — Surah Ar-Rahman 55:60
Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani
Verse 61 — Surah Ar-Rahman 55:61
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 62 — Surah Ar-Rahman 55:62
Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili
Verse 63 — Surah Ar-Rahman 55:63
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 64 — Surah Ar-Rahman 55:64
Za kijani kibivu
Verse 65 — Surah Ar-Rahman 55:65
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 66 — Surah Ar-Rahman 55:66
Na chemchem mbili zinazo furika
Verse 67 — Surah Ar-Rahman 55:67
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 68 — Surah Ar-Rahman 55:68
Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga
Verse 69 — Surah Ar-Rahman 55:69
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 70 — Surah Ar-Rahman 55:70
Humo wamo wanawake wema wazuri
Verse 71 — Surah Ar-Rahman 55:71
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 72 — Surah Ar-Rahman 55:72
Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema
Verse 73 — Surah Ar-Rahman 55:73
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 74 — Surah Ar-Rahman 55:74
Hajawagusa mtu wala jini kabla yao
Verse 75 — Surah Ar-Rahman 55:75
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 76 — Surah Ar-Rahman 55:76
Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri
Verse 77 — Surah Ar-Rahman 55:77
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Verse 78 — Surah Ar-Rahman 55:78
Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu